Linda Mshana Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self akitoa elimu kwa wananchi wa mkoa wa Arusha wlaiofika kwenye banda la taasisi hiyo ili kupata uelewa wa masuala ya mokopo.
………………………
Linda Mshana Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self amesema kuwepo kwao katika maonesho ya wiki ya taasisi za kifedha yanayofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kunatokana na moja ya majukumu yao ambayo ni kuelimisha Umma wa watanzania kuelewa umuhimu wa masuala ya Fedha ikiwemo kukopa Fedha kwa ajili ya biashara na maendeleo yao mengine
Amesema pia wananchi wanatakiwa kujua maswali muhimu ya kujiuliza kabla hujakopa fedha katika taasisi yoyote ya fedha, ni muhimu ukajua lengo lako la kukopa ni nini? na kwa ajili ya kufanyia nini? lakini pia wapi ukope na wakati gani ukope?.
Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye mikopo ya “Kausha Damu” bila kujijua wanajikuta tayari wameshakopa na wameingia kwenye matatizo na mali zao kuchukuliwa
“Tutakuelimisha ni vitu gani unatakiwa kuuliza kabla ya kuchukua mkopo kama vile na majibu unayopewa yanaweza kukuepusha na mikopo isiyo na tija wakati unapochukua haya mambo yote mkopaji anatakiwa kuyajua na kuwa na majibu sahihi kabla ya kuchukua mkopo” Amesema Linda
Self Microfinance inatoa Fursa mbalimbali ambazo zipo katika mfuko huo, Fursa hizo ni kama mikopo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati, Wafanyakazi wa taasisi za serikali , mikopo yaTaasisi zingine za kifedha pamoja na watu wanaotaka mikopo kwa ajili ya kuboresha makazi yao alafu tutakushauri ni mkopo gani utakufaa kukopa.
Jambo kubwa zaidi ni kwamba Self Microfinance inawahamasisha wakazi wote wa mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani ili waweze kufika katika banda la taasisi hiyo na kupata maelezo yatakayowapa uelewa wa namna ya kuweza kukopa na vitu muhimu vya kuwa navyo na kuvielewa kabla hujachukua mkopo.