Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Kaskazini Gradnnes Lema akiandaa taarifa ya kazi zake katika banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kwenye Wiki ya maonesho ya Taasisi za Kifedha jinink Arusha.
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Kaskazini Gladnnes Lema akimsikiliza Khadija Maulid Meneja Uhusiano na Mawasiliano TIRA katika banda la mamlaka hiyo jijini Arusha.
……………………….
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Kaskazini Gladnnes Lema, amesema wanaendelea kutoa elimu ya bima bule kwa wananchi ili wazidi kufahamu umuhimu wa kukata bima mbalimbali zitakazo wasaidia pindi wanapopata majanga.
Lema ameyasema hayo leo Novemba 22, 2023 alipokuwa akizungumza na Fullshangwe Blog kwenye maadhimisho ya wiki ya taasisi za kifedha Kitaifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya fedha kwa maendeleo ya kiuchumi”.
Amesema wanaliendeleza soko na kusimamia uhimilivu na uendelezaji wa Sekta ya bima ili kuweza kuielimisha jamii juu ya ukataji wa bima.
“Ikumbukwe pia taasisi yetu ni washauri wakuu wa Serikali kwenye mambo yote ya bima”, amesema Lema
Aidha, ameeleza kuwa wanasajili makampuni ya bima ambayo yanapokea majanga kutoka kwa wananchi, pia wanasajili mawakala wa bima ambao ni wawakilishi wa makampuni ya bima mbalimbali sanjari na washauri ambao kazi yao ni kuwashauri wateja ni bima gani wakate kutokana na mahitaji yao.
Ameeleza kuwa wanawasajili wakadiliaji wa hasara wa bima ambao ikitokea janga la kibima ndio wanaokwenda kwenye tukio wanafanya ukaguzi,ukadiliaji wa hasara wanashauri Kampuni ya bima ilipe kiasi gani kutokana na hilo janga.