Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko (wa Tatu
kulia) akikagua jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
katika Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma. Pamoja naye ni Katibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jimmy
Yonaz (wa kwanza kushoto) pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Wizara
ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

………
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko leo
amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba
jijini Dodoma.
Dkt.Biteko katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Katibu Mkuu, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jimmy Yonaz, na watendaji
mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.
Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko alikuta ujenzi
unaendelea ambao kwa sasa umefikia asilimia 69 ambapo Mkandarasi ni
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aidha ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na
Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na
Mkandarasi ni SUMA JKT.