Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bw. Maduhu Sayi Msekwa (kulia) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe katika viwanja vya Machinga Complex jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Mkuu wa Kanda ya Kati ya Vodacom Tanzania PLC, Joseph Sayi (kushoto) akikabidhi kiashiria cha bima ya afya kwa mmoja wa akina mama katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kupitia kampeni inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’ mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii jumla ya akina mama na watoto wachanga 2,000 watakabidhiwa bima kubwa ya afya kupitia VodaBima kutoka Vodacom itakayotumika kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kampuni hiyo kwenda kwa watanzania katika msimu huu wa sikukuu.
Masta Shangwe kutoka Vodacom Tanzania PLC, (katikati) akikabidhi kiashiria cha bima ya afya kwa Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, Dkt. Baraka Mponda – (kulia) na Muwakilishi Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Simon Chacha (kushoto) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kupitia kampeni inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’ mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii jumla ya akina mama na watoto wachanga 2,000 watakabidhiwa bima kubwa ya afya kupitia VodaBima kutoka Vodacom itakayotumika kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kampuni hiyo kwenda kwa watanzania katika msimu huu wa sikukuu.