Erasmus Fabian Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA akiwasilisha mada katika kikaokazi cha Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika Leo jijini Dar es salaam ambapo ameelezea malengo ya mfuko huo, mipango utekelezaji na mafanikio ya mamlaka hiyo.
Masozi Nyirenda Kaimu Mkurugenzi Utafutaji wa Rasilimali na Miradi Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA akielezea Miradi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo nchini wakati wa kikaokazi kati ya Mamlaka hiyo TEF na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
mwanahamisi Chambega Kaimu Mkurugenzi Huduma za Taasisi akifafanua baadhi ya mambo katika kikaokazi hicho.
…………………..
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Erasmus Fabian ameeleza kuwa kupitia kifungu cha 16 Cha sheria ya kodi ya mapato sura ya 332 inatoa haueni ya kodi kwa mtu ambae anaechangia elimu kupitia mfuko wa elimu.
Hayo ameyabainisha katika kikao kazi Cha jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na Ofisi ya msajili wa Hazina kilichofanyika leo Novemba 20, 2023 Jijini Dar_es_ salam na kueleza kuwa wao kama mamlaka ya mfuko wa elimu Tanzania watamtangaza mtu atakayeweza kuchangia elimu kupitia mfuko huo na pia watamuingiza kwenye daftari la kudumu la wachangiaji.
Fabian amesema kuwa mdau atakayeweza kuchangia elimu kupitia mfuko wa elimu atapata faida ya kupewa hati ya utambuzi kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha sheria ya mfuko wa elimu ya mwaka 2001.
“Mtu yeyote atakayeweza kuchangia elimu kupitia mfuko wa elimu atapata cheti ambacho anaweza kukipeleka kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitakachomsaidia kupata unafuu wa ulipaji kodi” Ameeleza Fabian.
Fabian amesema kuwa sheria inaitaka mamlaka ya elimu Tanzania kujenga ushirikiano na Taasisi za ndani na nje ya nchi kwa lengo la kushirikiana katika kuboresha elimu nchini,hivyo mamlaka inaushirikiano na taasisi mbalimbali kwenye kuchangia elimu na kuboresha elimu hapa nchini.
Aidha ameeleza kuwa Mamlaka inajukumu la Kufadhili miradi ya elimu ili kuinua kiwango cha ubora wa elimu na kuongeza upatikanaji wake kwa usawa kulingana na mipango na sera za Taifa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi.
“Hili ni kati ya jukumu kuu la mamlaka ya elimu Tanzania katika kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo uandishi wa maandiko kwa ajili ya kupata wafadhili, kuendeleza mahusiano na taasisi mbalimbali zinazoweza kuchangia kwenye mfuko wa elimu” Amesema Fabian.
Amefafanua kuwa Mamlaka inapokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi, watu binafsi na michango hiyo inaweza kuwa ya fedha au ya vifaa vikiwemo saruji, pamoja na mabati.