Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri akifungua mkutano wa wadau wa Uchaguzi kuhusu maanadalizi yua Uboreshaji wa Daftari la Kudumnu la Mpiga Kura Mkoani Tabora. Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni miongoni mwa Kata Mbili ambazo zitashiriki Uboreshaji wa Majaribio ambayo yanataraji kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Wadau mbalimbali wa Uchaguzi wakiwa katika Mkutano huo leo Novemba 20,2023.
Tume ya Taifa
ya Uchaguzi imewaasa wakazi wa maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya majaribio ya
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi kushiriki
kwenye zoezi hilo ambalo linalenga kupima utayari wa mifumo na vifaa vya
uboreshaji wa Daftari.

Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani
Tabora leo tarehe 20 Novemba, 2023 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.
Balozi Omar Ramadhan Mapuri amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa mkoa wao kuwa miongoni
mwa mikoa miwili ambayo kata zake zimeteuliwa kufanya majaribio hayo ambayo
yatafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.
Mhe. Mapuri
amezitaja kata zitakazofanya majaribio hayo kuwa ni Kata ya Ng’ambo iliyopo
katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, ya mkoa wa Tabora na Kata ya Ikoma
iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, katika Mkoa wa Mara.
“Tume
inawapongeza wakazi wa Mkoa wa Tabora kwa mkoa wenu kuteuliwa kuwa mwenyeji wa
zoezi hili la uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,”
amesema Mhe. Mapuri.
Ameongeza
kwamba uboreshaji wa majaribio kwenye kata hizo utafanyika katika vituo 16 vya
kuandikisha wapiga kura ambapo vituo 10 vipo katika Kata ya Ng’ambo na vituo
sita vipo katika Kata ya Ikoma.
Ameeleza
kwamba vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa
12:00 jioni.
Majaribio ya
uboreshaji yatahusisha kuandikisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au
zaidi na atakayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2025.
Kundi lingine
litakalohusika kwenye zoezi hili ni; wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao
wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo lingine, waliopoteza au kadi
zilizoharibika, wanaorekebisha taarifa zao na kuondoa wapiga kura waliopoteza
sifa za kuwemo katika Daftari.