Waziri wa Mifugo na uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza wakati alipofanya ziara yake wilayani Longido mkoani Arusha.
Mwekezaji wa kiwanda hicho cha Eliya food Overseas Ltd kilichopo wilayani Longido,Shabir Virjee akizungumza mbele ya Waziri wa Mifugo na uvuvi ,Abdalah Ulega
…….
Julieth Laizer ,Arusha .
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdalah Ulega,amewaagiza wataalamu wa Mifugo na mazao ya mifugo nchini, kusimamia sheria za mifugo ili kuhakikisha mifugo inayochinjwa kwa ajili ya biashara ya nyama iwe ni madume pekee huku wakiacha majike kwa ajili ya uzalishaji zaidi .
Ulega ameyasema hayo wakati alipofanya ziara yake katika kiwanda cha Nyama cha Eliya food Overseas Ltd kilichopo Longido mkoani Arusha ,kilichojengwa katika eneo maalumu la mauzo ya nje (EPZ) na kueleza kuwa kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda viwili vikubwa Tanzania vilivyopata fursa ya kuuza Nyama katika soko la nchini, Saud Arabia.
Amesema fursa hiyo imekuja kufuatia ziara ya rais Samia suluhu nchini Saud Arabia kwa mwaliko wa Mfalme wa Said Arabia na miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni suala la biashara ya uwekezaji, ambapo rais Samia alifanikiwa kuishawishi nchi hiyo kununua Nyama kutoka Tanzania.
Waziri Ulega amesisitiza kuwa suala la ubora wa nyama inayozalishwa hapa nchini ni kipaumbele cha biashara hiyo nje ya nchini , hivyo aliwataka wataalamu kusimamia sheria hizo kwa kuhakikisha mifugo inayochinjwa ni madume pekee ili kunusuru vizazi kwa kuchinja majike.
Amesema fursa hiyo imekuja kufuatia ziara ya rais Samia suluhu nchini Saud Arabia kwa mwaliko wa Mfalme wa Said Arabia na miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni suala la biashara ya uwekezaji, ambapo rais Samia alifanikiwa kuishawishi nchi hiyo kununua Nyama kutoka Tanzania.
Waziri Ulega amesisitiza kuwa suala la ubora wa nyama inayozalishwa hapa nchini ni kipaumbele cha biashara hiyo nje ya nchini , hivyo aliwataka wataalamu kusimamia sheria hizo kwa kuhakikisha mifugo inayochinjwa ni madume pekee ili kunusuru vizazi kwa kuchinja majike.
“Kwa Mara ya kwanza Tanzania tumefanikiwa kupata soko la kuuza Nyama Uarabuni baada ya rais Samia kufungua milango, walikuja wataalamu kutoka Saudi Arabia na kufanya ukaguzi wa viwanda vyetu vitano vya Nyama hapa nchini, lakini viwanda viwili vya Eliya food na Tan choice cha Mkuranga ndio vilifanikiwa kuchaguliwa”amesema .
Aidha amesisitiza kuwa ,pamoja na kwamba sheria ya Nyama hapa nchini inasisitiza uchinjwaji wa madume, pia soko la nchi hiyo linahitaji Nyama kutoka kwa mfugo dume.
Naye Mwekezaji wa Kiwanda hicho cha Eliya food, Shabir Virjee alimpongeza rais Samia kwa kufanikisha kufungua milango ya kuuza Nyama katika soko la nchi za Uarabuni ambapo kwa Miaka Mingi Tanzania ilikosa soko hilo.
Amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni ukosefu wa madume ya Mbuzi katika kukuza soko la Nyama ,kwani nchi za Uarabuni wanahitaji zaidi nyama ya mbuzi kutoka kwa mfugo dume .
“Changamoto nyingine ni bei ya nyama ya Ng’ombe kutoka Tanzania, tunashindwa kusafirisha Nyama ya Ng’ombe kwenda Uarabuni kwa sababu nchi za India na Australia wanauza nyama ya Ng’ombe nchini humo kwa bei rahisi na hivyo kuharibu somo la Nyama”.amesema .
Aidha Virjee, ameiomba serikali kuwaruhusu kuuza soko la ndani tani 15 ya Nyama ambayo haiwezi kusafirishwa kwenda nje ya nchi iliyotokana na masalia .
“Tuna tani 15 ya Nyama( reject) ambayo tunayo kiwandani ambayo haiwezi kusafirishwa nje ya nchi na hii Nyama ilitokana na baadhi ya mifugo kulalia upande kwa muda mrefu au kupata majeraha ya aina yoyote ikiwemo kupigwa”amesema Virjee.
Hata hivyo Waziri Ulega alipokea ombi hilo na kumtaka Mkurugenzi wa kiwanda hicho kuiandika barua serikali na kuielekeza kwake ili aifanyie kazi ikiwemo ombi la kusamehewa ushuru waweze kuuza kiasi hicho cha Nyama katika soko la ndani kuliko kuteketezwa kwa moto.