Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa William Samoei Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya leo tarehe 19 Novemba, 2023 Ikulu, Nairobi.
Rais Mstaafu Kikwete ambaye ni Mlezi wa Jukwaa la Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (YouLead Summit) pamoja na mambo mengine, alifika Ikulu ya Nairobi kumjulisha Mheshimiwa Rais Ruto juu ya masuala mbalimbali ya Mkutano wa Jukwaa hilo unaotarajiwa kuanza kesho jijini Nairobi.