Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea na kukagua Hospitali ya wilaya ya Muhez
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera akitembelea maeneo mbalimbali katika Hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera akikagua hali ya upatikanaji wa dawa wakati alipotembelea Hospitali ya wilaya ya Muheza
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera akikagua hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya wilaya ya Muheza
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera amefanya ziara ya kutembelea na kukagua hospitali ya wilaya ya Muheza huku kieleza kwamba kwa wale watakaobainika walifanya uzembe wilayani Handeni watachukuliwa hatua kali ikiwemo kunyang’anya leseni.
Dkt Mahera aliyasema hayo mara baada ya ziara hiyo ambapo alisema kwamba Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya ili wananchi wapate huduma bora hivyo wao hawatakubali kuona watumishi wanakiuka maadili.
Alisema hivyo lazima watumishi wabadilike waache kufanya kazi kwa mazoea na vitendo hivyo visijirudie kwani kufanya hivyo kunapelekea kuzorotesha huduma hivyo niwasihi muendelee kutoa huduma nzuri na kufanya kazi kwa waledi katika kuwahudumia wananchi.
Dkt Mahera alisema yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa madaktari wa meno hivyo akaona apite katika Hospitali hiyo kuangalia huduma za afya kutokana na kwamba Serikali ya imewekeza fedha nyingi kuwekeza kwenye sekta ya afya ikiwemo miundombinu.
“Kwa kweli niwapongeze mnaosimamia mradi huu wa Hospitali ya wilaya ya Muheza changamoto niliyoiona hapa ni maji Hospitali ya wilaya kama hii inapata maji kutoka Tang tumekagua maabara maji hakuna bahati nzurti mmechimba kisima na halmashauri imenunua pamp niagize mkamilisha haraka miuondombinu ya maji iweze kuingia kwenye maabara”Alisema Dkt Mahera
“Lakini pia watumishi fanyeni kazi kwa waledi na kujituma na kuendelea kuhakikisha watoto njiti pale wanapojitokeza waendele kuboresha huduma hizo kwenye maeneo yenu kama nchi tumepata mafanikio makubwa sana kuzuia vifo vinavyotokana na mama na mtoto.
Hata hivyo alisema kwamba katika bajeti ya mwaka kesho wataangalia namna ya kupata fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ambao ni muhimu kwa ajili ya utoaji huduma
“Mh Rais Dkt Samia Suluhu amekuja na mpango wa M-Mama ili mama anapohitaji huduma ya Rufaa anaipata na niwaambie kwamba kwa wale kwa wale ambao watabainika wanafanya kazi kwa mazoea na kukiuka maadili hatutawavumilia tutaendelea kuwachukulia hatua kali “Alisema
Hata hivyo alisema kwamba miaka 5 iliyopita walikuwa na Hospitali za wilaya 77 sasa zipo 177 za Serikali hivyo hilo ni jambo la kujivunia sana na huduma zinazotolewa kwenye hospitali hizo ni za msingi unakutana na huduma mbalimbali muhimu.