Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya,Tiba na Sayansi slShirikishi MUHAS Profesa Apolinary Kamuhabwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki matembezi maalum ya kuchangia bunifu za watafiti wa mascara tiba na magonjwa.
Rais wa idara ndogo ya waliohitimu , wanaendelea kusoma na wanaofanyakazi MUHAS Marsha Yambi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki matembezi maalum ya kuchangia bunifu na tafiti kuhusu tiba na magonjwa.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya,Tiba na Sayansi slShirikishi MUHAS Profesa Apolinary Kamuhabwa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kwa wanawake mara baada ya kushinda mbio hizo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya,Tiba na Sayansi slShirikishi MUHAS Profesa Apolinary Kamuhabwa akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi wa mbio hizo Nora Malmin.
……………………………..
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya,Tiba na Sayansi slShirikishi MUHAS Profesa Apolinary Kamuhabwa amewataka wadau mbalimbali kuendelea kusaidiana na kushirikiana katika kuendeleza tafiti na bunifu ili kuboresha afya za wananchi.
Hayo ameyasema leo Novemba 18, 2023 jijini Dar es Salaam baada ya kukamilisha matembezi ya kujifurahisha(Fun Run) yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuendeleza tafiti yaliyohusisha wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliosoma chuoni hapo miaka iliyopita.
Amesema katika matembezi hayo yaliyohusisha mbio za Km1, Km5, Km10 na Km15 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 10 ambazo zitakwenda kuendeleza tafiti na bunifu hasa zinazofanya na wanafunzi chuo hapo.
“Matembezi haya tumeyafanya lengo kubwa ni kuhamasisha ubunifu ambapo kwa leo tumekusanya shilingi milioni10 na fedha hizo zinapelekwa kwenye kitengo cha bunifu na tafiti”amesema profesa Kamuhabwa.
Aidha ameongeza kuwa katika kitengo hicho cha bunifu na tafiti chuoni hapo wanahamasisha watumishi,wanafunzi na watu wengine ambao ni wana bunifu zao kuzipeleka kwenye kitengo hicho ili ziweze kusajiliwa na kuwatafutia wadau kwa ajili ya kuendeleza bunifu zao.
Amesema wanaendelea kuimarisha kitengo hicho kwani kuna vijana wengi wenye uwezo mkubwa Sana na wenye bunifu hivyo wanataka vijpaji hivyo kuvikuza na kuleta bunifu ambazo zitasaidia nchi.
“Bunifu nyingi zinazofanywa na vijana wetu ni zile ambazo zinalenga kwenda kusaidia mfumo wa afya kwenye kuchunguza,kutibu na kuangalia mifumo yetu ya afya na sasa hivi teknolojia imeenda mbali sana sasa hivi vijana wamewekeza kwenye akili bandia hivyo tunaamini kitengo hiki kikiimarika kitatusaidia sana”amesema.
Aidha Profesa Kamuhabwa ametoa rai kwa wananchi kuacha tabia bwete na kujikita kwenye mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza Kama Kisukari,Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo ambayo yanasababishwa na mtindo wa maisha.
Kwa upande wake Rais wa idara ndogo ya waliohitimu , wanaendelea kusoma na wanaofanyakazi MUHAS Marsha Yambi amesema wao wanamipango mingi ikiwa Kama sehemu ya fadhila kwa chuo chao ili kukufanya chuo hicho kuwa Bora na cha mfano kwa taifa.
Amesema Dunia ya sasa ni ya kutafuta majawabu hivyo fatiti na bunifu lazima ziwe zenye kuleta mabadiliko chanya ili kuhakiksha uendelevu wa afya katika taifa.
“Dunia ya sasa sio ya kukopi na kupesti ni Dunia ya kutafuta majawabu na majawabu hayo yanatafutwa kwa kujaribu hivyo watafiti lazima wawe wabunifu wa changamoto mbalimbali kwa kutengeneza majawabu ya kuleta mabadiliko chanya ambapo kwa kufanya hivyo tutaendelea kupunguza yale yaliyokuwa Kero kama vifo vya mama na watoto,magonjwa yasiyoambukiza na yakuambukiza”amesama Yambi.