Na.Joctan Agustino,NJOMBE
Mahakama kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya hakimu mkazi Njombe ambayo ililikuta Kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kusinina hatia baada ya gari lake kusababisha ajali ambayo ilipelekea kifo cha Kaselida Mlowe eneo la Ruhuji Mjini Njombe ambaye ameacha watoto watatu waliyokuwa wakimtegemea.
Akisoma hukumu ya kesi no 12,2023 ya rufaa Maximilian Maleo ambaye ni msajili wa mahakama kuu Kanda ya Iringa amesema mahakama imepitia sababu zote 10 zilizotolewa na upande wa mdaiwa na kujiridhisha kwamba hazina mashiko na kisha kuagiza upande wa mdaiwa ambaye ni kanisa kulipa pia ghalama za kesi hiyo.
Ikumbukwe kwamba kesi hiyo ya rufaa ambayo imetupiliwa mbali na mahakama kuu ya Iringa ilifunguliwa na Kanisa baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe Lihad Chamshama ambapo kanisa lilihukumumiwa kulipa fidia ya milioni 70 kutokana na uzembe uliofanywa na mdaiwa namba moja bwana Rajab Kitwana aliyekuwa dereva wa gari la kanisa aina Mercedes Benz Track lenye NO za usajili T 210-AHU mali ya kanisa kusababisha ajali katika Mlima Ichunilo mjini Njombe Septemba 25,2020 iliyopeleka kifo cha Kaselida Mligo baada ya kugongana na gari la abiria aina Hiace lenye Namba za usajili T 298 DNE.
Msimamizi wa mirathi wa Marehemu Kaselida Migo Bi Sigrada Mligo alifungua kesi No 2 ya mwaka 2022 ya madai ya fidia ya Milioni 100 kutoka kanisa la KKKT na lakini mahakama ya hakimu mkazi Njombe kusikiliza Ushahidi kutoka pande zote mbili na kisha kutoa hukumu ya fidia mil 70 ambapo nayo Upande wa mdaiwa ambaye ni kanisa hakuridhia na kuamua kufungua kesi ya rufaa katika mahakama kuu kanda ya Iringa ambako nako Limepoteza baada ya mahakama kudai sababu zilizotolewa hazina mashiko.
Katika kesi hiyo upande wa madai uliwakilishwa na mawakili watatu akiwemo Emmanuel Chengula,Frank Ngafumika na Gervas Semgabo huku upande wa utetezi ambaye ni mdaiwa ukiwakilishwa na wakili Marco Kisakali ambapo hadi umauti unamkuta Bi Kaselida Mligo.