Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Ramadhani Kailima akiwasilisha mada katika mkutano wa kitaifa wa tume ya uchaguzi na vyama vya siasa kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu wa wapiga kura unaofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar SalaamSalaam.
……………………..
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeboresha mfumo wa uboreshaji wa taarifa za mpiga kura ambapo sasa mpiga kura anaweza kuboresha taarifa Zake kwa kutumia simu au kompyuta.
Akizungumza jijini Dar es salaam Novemba 16,2023 wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa kitaifa wa tume ya uchaguzi na vyama vya siasa kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu wa wapiga kura unaofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Salaam, Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Ramadhani Kailima amesema mfumo huo unaofahamika kama OVRS baada ya kuuboresha ule wa awali wa BVR ambapo sasa OVRS ndiyo utakaotumika kuboresha taarifa za mpiga kura ambaye tayari alishaandikishwa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
“Mfumo huu wa OVRS hautawahusisha ambao wanaanza kujiandikisha huu ni kwa wale walio kwishajiandikisha sasa wanataka kuboresha taarifa zao”amesema Kailima
Akizungumzia kuanza kwa zoezi la uandikishaji wa daftari kwa mikoa miwili wa Tabora na Mara ambayo ina mwingiliano mkubwa wa watu amesema wataanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kuandikisha huko kutokana kuwa na mwitikio mkubwa wa wapiga kura lakini pia kuwa karibu na nchi jirani.
Amesema zoezi litafanyika kwa siku saba kuanzia Novemba 24 mpaka Novemba 30,2023 katika kata ya Ng’ambo ilipo katika Halmashauri ya manispaa ya Tabora mkoa wa Tabora na kata Ikoma iliyopo halmashauri ya Rorya mkoani Mara .
“Sababu ya kuchagua maeneo hayo ni ongezeko kubwa la watu katika maeneo hayo lakini hali ya miundombinu ya mawasiliano na muingiliano wa watu kutoka nchi jirani lakini eneo moja wapo lipo maeneo ya mpakani hivyo mwingiliano ni mkubwa “amesema.
Amesema katika kata ya Ng’ombo pamoja na kuwa na vituo 10 vya uchaguzi lakini kuna muitikio mkubwa wa watu kujiandikisha kupiga kura mwaka 2020 walijiandikishwa na kuboresha daftari walikua 9435 sawa na ongezeko la asilimia 14.64.
Ameongeza kuwa katika kata hiyo kuna idadi kubwa ya wapiga kura kwa mujibu wa takwimu za Sensa kata hiyo ina watu 17829 na makadilio ya wapiga kura ni 10940 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la watu1205 sawa na ongezeko la asilimia 12.77 ya waliojiandikisha mwaka 2020.
Aidha Kailima amesema kuwa uboreshaji wa daftari hilo utatoa fursa ya wapiga kura kuboresha taarifa zao lakini waliopoteza au kuharibi kadi zao kupatiwa kadi mpya hapo hapo lakini pia litatoa fursa ya kuwaondo wale waliopoteza sifa ya kuwa wapiga kura.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Jaji Jacobs Mwambegeja kushoto akiwa na Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Ramadhani Kailima wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa tume ya uchaguzi na vyama vya siasa kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu wa wapiga kura unaofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Time ya U chaguzi wakiwa katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Viongozi kutoka chama cha ACT Wazalendo wakiwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika akiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya maafisa wa vyonbo vya ulinzi na usalama waneshiriki pia katika mkutano huo.
Baadhi ya maofisa kutoka Tume ya taifa ya u chaguzi
Dkt. Jim James Yonazi. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu kushoto pamoja na viongozi wengine wakiwa katika mkutano huo.