Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam (Mradi wa Maji Bangulo) iliyofanyika leo Novemba 17,2023 katika Kata ya Pugu, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Bw. Kihula Kingu pamoja na Mkandarasi M/S Sinohydro kutoka nchini China wakiweka saini ya makubaliano ya wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam (Mradi wa Maji Bangulo) iliyofanyika leo Novemba 17,2023 katika Kata ya Pugu, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Bw. Kihula Kingu akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam (Mradi wa Maji Bangulo) iliyofanyika leo Novemba 17,2023 katika Kata ya Pugu, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Maji Mhe. Marry Prisca, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Bw. Kihula Kingu wakimpokea Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso baada ya kuwasili katika Viwanja vya Pungu Stesheni kwa ajili ya kushuhudia utiaji saini wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam (Mradi wa Maji Bangulo)
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakiwa katika hafla ya utiaji saini wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam (Mradi wa Maji Bangulo) iliyofanyika leo Novemba 17,2023 katika Kata ya Pugu, Jijini Dar es Salaam.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeingia makubaliano na Mkandarasi M/S Sinohydro kutoka nchini China kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam ( Mradi wa Maji Bangulo) wenye thamani ya Shilingi bilioni 42.
Mradi huo unatekelezwa na (DAWASA) kwa ufadhili wa benki ya Dunia ambao unatarajiwa kunufaisha wananchi 450,000 katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza leo Novemba 17, 2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameziagiza Mamlaka za Maji nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu kwa ufanisi ikiwemo kuwaunganishia maji wananchi wenye uhitaji kwa mkopo.
Mhe. Aweso amesema kuwa mwananchi akiomba huduma ya maji anapaswa kuunganishiwa ndani ya wiki mbili ili aweze kupata huduma hiyo muhimu.
“Mwananchi akishindwa kumudu gharama za kuunganishiwa maji anapaswa kukopeshwa na atakuwa analipa kidogo kidogo wakati analipa bili ya maji” amesema Mhe. Aweso.
Mhe. Aweso ameipongeza DAWASA pamoja Bodi yake kwa kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija kwa serikali katika utekelezaji wa majukumu ya kutoa huduma ya maji.
“DAWASA nawapongeza kwa kazi nzuri, pia naomba msimamie mradi huu utatekelezwa na kumalizika kwa muda ambao jmekusudiwa kulingana na mkataba ” amesema Mhe. Aweso.
Amesema kuwa mkakati wa serikali ni kusambaza maji kwa asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 kwa vijijini ifikapo 2025.
Mhe. Aweso amesema kuwa upatikanaji wa maji mwezi Julai 2022 hadi Juni 2023 kwa mjini umepanda kwa wastani asilimia 88 na inatarajia kufika asilimia 91 mwezi Desemba 2023, huku akieleza kwa vijijini huduma imeongezeka kutoka asilimia 77 na inatarajiwa kufika asilimia 80 mwezi Desemba, 2023.
Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA Bw. Kihula Kingu amesema kuwa mradi huo utanufaisha wananchi wa Wilaya tatu za Ubungo, Temeke na Ilala na majimbo manne ya uchaguzi Ukonga, Segerea, Ubungo, Kibamba na Ilala.
Amesema, awamu ya kwanza ya mradi itanufaisha wananchi wa Kata za Kwembe, Kitunda, Pugu Stesheni, Kipunguni na Mzinga.
Awamu ya pili ya mradi itanufaisha wananchi wa Kata ya Kivule, Kinyerezi, Zingiziwa, Majohe, Charambe, Kwembe, Buza, Msongola, Msigani na Mbezi.
Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji kusini mwa Dar es Salaam unahusisha ulazaji bomba la chuma la kusafirishia maji kwa umbali wa kilomita 10.8 kutoka kwenye Kituo cha kusukuma maji Kibamba mpaka kwenye tanki la Bangulo.
Ujenzi wa tanki la kuhifadhi na kusambaza maji litakuwa na ukubwa wa lita 9,000,000 litakalojengwa eneo la Bangulo, Kata ya Pugu, huku mradi huo unatarajiwa kuzalisha mita za ujazo 23, 333 mwa siku.
Mradi huo unatarajiwa kutekeleza kwa muda wa miaka miwili kuanzia Oktoba 2023 hadi Oktoba 2025, huku chanzo cha maji katika mradi ni mitambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu.