Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe. Omar Dadi Shajak akiwasilisha ripoti ya utekelezaji ya kipindi cha kuanzia Julia hadi Septemba 2023 mbele ya wajumbe wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya (B.L.W ),huko Ofisi za Mamlaka ya Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya (B.L.W ),Mhe.Machano Ali Said akizungumza na watendaji wa Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha kuanzia Julia hadi Septemba 2023 huko Ofisi, za Mamlaka ya Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.
Mjumbe wa kamati ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa Kitaifa Haji Shaabani Waziri akiuliza maswali kwa watendaji wa Ofisi ya mamaku wa kwanza wa Rais juu ya ripoti yao ya utekelezaji kwa kipindi cha Julia hadi Septemba 2023 huko Ofisi ya Mamlaka za Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.
Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi kuu za Viongozi wa Kitaifa Maryam Thani Juma akiuliza swali kuhusiana na ripoti ya utekelezaji kwa watendaji wa Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais mara baada ya kuwasilishwa ripoti hiyo huko Ofisi za Mamlaka ya Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Ukimwi Zanzibar Dkt. Ahmed Mohammed Khatib akijibu maswali ya wajumbe wa kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa kuhusiana na hali ya Ukimwi wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji kuanzia julai -September 2023,huko Ofisi za Mamlaka ya Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Omar Dadi Shajak akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya (B.L.W) kupokea taarifa ya utekelezaji ya Ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia julai hadi Septemba 2023, huko Ofisi za Mamlaka ya Mazingira Maruhubi Mjini Unguja.
……….
Imani Mtumwa Maelezo 16/11/2023
Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeridhishwa na utendaji kazi wa Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais .
Akizungumza mara baada ya kupokea Taarifa ya utekelezaji iliyoanzia Julai hadi Septemba 2023, Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongonzi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Mhe,Machano Ali Said alisema taarifa hiyo imeonesha kufanya vyema katika Taasisi zote zilizopo chini ya Ofisi hiyo.
Amesema Ofisi hiyo imekuwa ikifanyakazi kwa mashirikiano na wadau na Taasisi mbalimbali kwa maslahi ya Wananchi.
Hivyo aliishauri Serikali kuiongezea nguvu Ofisi hiyo kwa kuweka vifaa vya kisasa katika njia za usafirishaji ili kuzuia uingiaji wa madawa ya kulevya yanayoenda kuharibu Vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Mhe.Mwenyekiti aliwashauri watendaji wa Ofisi hiyo kuhakikisha wanazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu wakati wanapojenga majengo mapya na kuongeza nguvu na kupiga vita suala la watu wenye ulemavu kuombaomba.
Hata hivyo aliitaka Tume ya Ukimwi kuzidi kutoa Elimu ili kuepusha mambukizi mapya.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi mitatu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Omar Dadi Shajak alisema kwa kipindi cha miezi mitatu wamefanikiwa kutekeleza miradi mitano ya maendeleo ikiwemo minne ya mazingira na mradi mmoja wa kituo cha tiba na kurekebisha tabia.
Alieleza kuwa jumla ya tani 105 za mchele na tani 16 za dawa na Vipodozi zilizopitwa na muda wa matumizi ziliangamizwa kwa kushirikiana na Wakala wa Dawa Chakula na vipodozi kwa lengo la kumlinda mtumiaji.
Aidha Ofisi hiyo imefanikiwa kutoa elimu ya ushauri nasahi na tiba ya Saikolojia kwa waraibu kupitia Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Zanzibar School of Health (SHAA) ili kusaidia wahanga hao kuondokana na tatizo hilo.
Pia alisema Ofisi imefanya ukaguzi katika miradi mitano ya maendeleo kwa lengo la kuangalia mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu .
Hata hivyo alisema Ofisi inakabiliwa na changamoto ya mashirikiano finyu kwa baadhi ya jamii kwa kuwa na muhali wa kutoa taarifa za watumiaji madawa ya kulevya sambamba na watu kutoelewa vyema kuhusiana na walemavu.