Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki akielezea maendeleo ya Taasisi hiyo tangu kuanzishwa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akichangia mada wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Manunuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Victor Kapama akielezea mchakato wa manunuzi unavyotakiwa kufuatwa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akijibu hoja zilizohusu idara yake wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es
Wagonjwa 32,867 watu wazima 30,616 na watoto 2,251 wenye matatizo mbalimbali ya moyo wamepata huduma ya matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akisoma taarifa ya kazi zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 katika mwaka wa fedha wa 2023/24 katika kikao cha wafanyakazi wa JKCI kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema wagonjwa waliolazwa walikuwa 1,131 kati ya hao watu wazima walikuwa 1030 na watoto 101.
“Kupitia mtambo wa Cathlab ambayo ni maabara inayotumia mionzi maalumu kwaajili ya uchunguzi wa matatizo na tiba za magonjwa ya moyo wagonjwa 638 watu wazima 630 na watoto nane walipata huduma za uchunguzi, kuzibuliwa mishipa ya damu ya moyo iliyoziba pamoja na kupandikizwa vifaa visaidizi vya moyo”, .
Wagonjwa 129 ambao ni watoto na watu wazima walifanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kubadilishwa valvu, kupandikizwa mishipa ya damu ya moyo (Coronary artery bypass grafting – CABG), kukarabati mishipa ya damu ya moyo iliyotanuka au kuchanika, kuziba matundu ya moyo, kutoa uvimbe katika kifua au mapafu, kupandikiza na kuzibua mishipa ya damu ya miguu.
Dkt. Kisenge alisema kwa kipindi hicho cha miezi mitatu waliona wagonjwa 61 kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Visiwa vya Comoro, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nje ya Africa ambazo ni nchi za Canada, Ufaransa na India.
“Tulifanya vipimo 14,864 vya jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) na mfumo wa umeme wa moyo (ECG), X-Ray 3,815 zilifanyika, vipimo vya maabara 7,966 na ultrasound 1,881 zilifanyika pia dawa zilitolewa kwa wagonjwa 30,249”, alisema Dkt. Kisenge.
Mkurugenzi huyo Mtendaji aliwakumbusha wafanyakazi wa JKCI kumtanguliza Mungu mbele katika kazi zao za kila siku huku wakiiombea taasisi hiyo ili iweze kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaowatibu.
Dkt. Kisenge alisema kutokana na huduma bora inayotolewa katika Taasisi hiyo imekuwa kivutio cha wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi kutaka kutibiwa hapo na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuimarisha huduma za matibabu ya moyo nchini.
Kwa upande wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo waliohudhuria mkutano huo waliishukuru menejimenti ya JKCI kwa kuwaongoza vizuri na kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata maslahi yao kwa wakati.
“Kuna watu wengi wanaohitaji kupata huduma za matibabu ya moyo tunazozitoa, ni jukumu letu kama Taasisi kutangaza huduma zetu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi”, alisema Jilala John ambaye ni Afisa Uuguzi katika Taasisi hiyo