Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph John Kilangi akizungumza kuhusiana na upatikanaji wa huduma za Nisahati Mbadala Zanzibar katika Warsha ya wadau wa maendeleo iliyofanyika Verde .
Naibu Waziri Wizara ya Maji, Nishati na Madini Shabaan Ali Othman akizungumza kuhusiana na upatikanaji wa huduma za Nisahati Mbadala Zanzibar katika Warsha ya wadau wa maendeleo iliyofanyika Verde .
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini wakiwa katika warsha ya kujadili changamoto za upatikanaji wahuduma za nishati mbadala kilichofanyika Verde.
Baadhi ya Wadau wa maendeleo wakiwa katika warsha ya kujadili changamoto za upatikanaji wahuduma za nishati mbadala kilichofanyika Verde.
……………………..
Na Fauzia Mussa , Maelezo
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kutekeleza mipango ya upatikanaji wa nishati mbadala kwa maendeleo endelevu Nchini.
Akizungumza katika warsha na wadau wa maendeleo huko Verde
Naibu Waziri, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Shabaan Ali Othman amesema
ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika upatikanaji wa huduma za umeme miradi mikubwa inahitajika ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa nishati hiyo.
Alisema vyanzo Mbadala vya umeme ni kipaombele kwa Zanizbar ambapo utekelezaji wake unakwenda kwakasi kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo,
Hivyo uwepo wa wadau wa maendeleo utaisaidi upatikanaji wa mambo mbalimbali ya kurahisisha utendaji katika Wizara hiyo ikiwemo upatikanaji wa fedha , vifaa pamoja na kuongezewa utaalamu wa kuendesha huduma hizo .
Hata hivyo alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuongeza nguvu katika Wizara hiyo kwa lengo la kuhakiksha Wizara inafanikiwa kutoa huduma za umeme wa uhakika, maji ya kutosha na madini yanayofikika kwa kiwango kikubwa .
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Joseph John Kilangi amesema kikao hicho kati ya watendaji wa ZESTA na Wizara hiyo kina lengo la kuangalia mafanikio yaliyofikiwa na changamoto wanazokabiliana nazo katika kufikisha huduma za nishati Mjini na Vijijini.
Alisema awali Zanzibar ilikua ikikabaliwa na changamoto za upelekaji wa huduma za umeme vijijini ambapo kwa sasa kupitia wadau wa maendeleo vijiji vingi vimefikiwa na huduma hiyo.
Alifahamisha kuwa kwasasa Wizara imejikita katika kuongeza upatikanaji wa huduma ya nishati hiyo katika sekta za maendeleo ikiwemo Utalii,Uchumi wa Buluu na Kilimo.
“Uchumi wa buluu ni ulimaji wa mwani,ufugaji na uvuvi wa samaki ,bila ya umeme adhma ya uchumi wa buluu hatuwezi kuifikia tunataka kuhakikisha umeme unamfikia kila mtu kwa gharama nafuu watu wote wanaojikita na utalii wanafikiwa na umeme wa kutosha na vijijini harakati za umwagiliaji kwaajili ya kuongeza kilimo”.alifahamisha katibu huyo
Amesema adhma ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi na wadau wa maendeleo ni kumrahisishia mwananchi kupata huduma za umeme kwa gharama nafuu.
Nao baadhi ya Wadau wa maendeleo wamesema wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia wizara hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.
Mkutano huo ni wapili kufanyika tangu kuanzishwa kwa mradi wa ZESTA kwa lengo la kuangalia na kujadili changamoto wanazokabilaiana nazo na kuzipatia ufumbuzi.