Akizungumza jijini Mwanza Katibu wa NEC Siasa, Itikadi Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda Amesema Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Chongolo walishaweka misingi ya Chama ili kiwe na Miradi ambavyo itakifanya chama kujisimamia na kujilipa mishahara._
Ndg. Paul Makonda ameyasema hayo alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa CCM wa nyumba 6 (Full Furnished Appartiments) ambapo kati yake nyumba nne ni za chini na nyumba mbili ni za ghorofa moja moja mradi upo jirani na Ikulu ndogo ya Jijini Mwanza.
Hadi kukamilika kwake miradi huo utagharimu kiasi cha shilingi Milion 687 ambapo vyanzo vya fedha ni mapato ya ndani ya CCM Mkoa, Wanachama , Wadau na Wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi na hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 41%.
Makonda akiwa akiwa katika eneo la mradi huo ameahidi kuleta lifti kwa ajli ya kuwekwa kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza lenye ghorofa 5.
Aidha, Mwenezi Makonda amesema kwakuwa yeye ni Mwenyekiti na RC Makalla ni Mhasibu katika ujenzi huo, hivyo wataandaa hafla ya chakula cha pamoja ambapo kupitia kadi za mwaliko katika hafla hiyo utawekwa wito wa kuchangia ujenzi kwa ajili ya kumalizia nyumba za mradi huo.
“Chama kikiwa na uwezo wa kiuchumi heshima yake inakuwa kubwa, wakati mwingine tunapata Viongozi wala rushwa kwa sababu walianza kuweka hela zao taratibu taratibu mwisho wa siku unashangaa Katibu yupo mifukoni mwa mtu kila likija jambo kanuni inapindishwa kwahiyo ni lazima tuwe na uchumi wetu wenyewe ili tujitegemee wenyewe” Alisema Mwenezi Makonda.