Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na kuwaelezea Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya nchini Morocco na Saudi Arabia. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Novemba, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya nchini Morocco na Saudi Arabia. Mkutano huo umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Novemba, 2023.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya nchini Morocco na Saudi Arabia. Mkutano huo umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Novemba, 2023.
……………………..
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepata jukwaa sahihi la kutangaza fursa ya uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali utakaochangia kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yameelezwa leo Ikulu jijini Dar es salaam katika mkutano wa waandishi wa habari na Mawaziri wa kisekta na wakurugenzi ulioitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus kuhusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyofanya nchini Morocco na Saudi Arabia.
Akizungumza katika mkutano Zuhura amesema kuwa sekta zilizopewa kipaumbele katika jukwaa hilo ni pamoja na sekta za viwanda,Madini,Nishati,na Usafirishaji pamoja na utunzaji wa Mazingira.
‘Mhe Rais aliweza kuhutubia siku ya ufunguzi nchini MOROCCO ambapo pia alilenga na kuelezea umuhimu wa ujenzi wa reli kutoka Mtwara-Mbabay na matawi ya Liganga na mchuchuma yenye urefu wa kilomita 1000 ikiwa ni lengo kunadi miradi ili kupata fedha ya kuendeleza miradi hiyoi’amesema Zuhura
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega amesema kuwa ziara hiyo imeongeza mashirikiano ya kibiashara katika usafirishaji wa bidhaa za nyama kwenda nje ya nchi.
‘Saudia pekee ambayo ilikuwa haichukui hata tani moja ya nyama kutoka Tanzania mpaka mwezi Juni mwaka huu wamekwisha kununua Tani 1400 na mahitaji yao yanafika mpaka tani 20000 kwa mwezi mmoja’amesema Waziri Ulega
Aidha Waziri Ulega amesema ni vyema wafugaji kuepuka kufuga kizamani kwa kimila bali kila anayefuga afuge kwa malengo ya kupata fedha.
Naye Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande amesema kuwa wawekezaji wengi katika nchi hizo wameonesha nia ya kuja Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali.
‘Zile fedha ambazo zimepatikana na hizi ambazo tunatarajia kuzipata zitakumika kwa usahihi na thamani ya pesa halisi itakayopatikana’amesema Chande
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya amesema Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan amekuwa ni mfano kwa marais wa nchi nyingine kutokana na kuonyoshe njia katika masuala ya kimaendeleo na kuwavutia wawekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania –TRC Masanja Kadogosa ameelezea maendeleo ya mradi wa reli na mafanikio huku Mkurugenzi wa Uhamasishaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania –TIC John Mnali akisema dhamira yao ni kuendelea kusimamia vyema na kuratibu suala la uwekezaji nchini.