Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuelekea kukagua uzalishaji wa maji safi ya kunywa ikiwa ni ziara ya kamati hiyo kukagua miradi mbalimbali katika Wizara ya Ulinzi.Ziara hiyo imefanyika eneo kilichopo kiwanda hicho JKT Mgulani, jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Victor Kawawa(wapili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa,Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa ziar ya kukagua uzalishaji wa maji safi ya kunywa katika kiwanda cha SUMA JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua chupa ya maji safi ya kunywa yanayotengenezwa katika katika Kiwanda cha Maji cha SUMA JKT Mgulani, jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajab Mabele. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imetembelea kiwanda hicho katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali iliyoko chini ya Wizara ya Ulinzi.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa,Meja Jenerali Rajab Mabele akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama kutembelea Kiwanda cha Maji Safi cha SUMA JKT kilichopo Mgulani,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama baada ya ziara ya kukagua Uzalishaji wa Maji Safi ya Kunywa ikiwa ni ziara ya kamati hiyo kukagua miradi mbalimbali katika Wizara ya Ulinzi.Wanne kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo,Victor Kawawa na wakwanza kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajab Mabele.Ziara hiyo imefanyika eneo kilichopo kiwanda hicho JKT Mgulani, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi