Na Sophia Kingimali
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka mawaziri wa fedha na mawaziri wa maendeleo ya jamii kwa nchi za Afrika kuimarisha mipango ya maendeleo ili kuimarisha haki za kiuchumi za wanawake katika Bara zima la Afrika.
Hayo ameyasema leo Novemba 15,2023 jijini Dar es salaam kwenye hoteli ya Rotana wakati akifungua mkutano wa mawaziri wa Afrika kuhusu uwekezaji kwa maendeleo ya usawa wa jinsia.
Amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejitolea kushughulikia kukosekana kwa usawa wa kijinsia kwa vitendo katika nyanja zote za mwanamke.
“Kipengele cha jinsia kimejumuishwa kikamilifu katika mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano(2021/22-2025/26)na dira ya maendeleo ya Tanzania 2025 ambayo yote yanasisitiza dhamira ya nchi katika kukuza usawa wa jinsia katika kijamii,kiuchumi na kisiasa”amesema Dkt Mwinyi.
Amesema sera zote za ubaguzi wa kijinsia zinapaswa kuondolewa na kupitisha na kutekeleza sheria na sera na kuweka mikakati ya uwekezaji ili kuwezesha upatikaji wa haki za wanawake na wasichana.
Aidha Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa mabadilko ya tamaduni yanapaswa kuingiliwa ili kubadilisha kanuni za kijamii zinazoleta au kuchochea ubaguzi.
Sambamba na hayo Dkt Mwinyi amesema Tanzania imepiga hatua katika kuongeza upatikanaji wa huduma fedha kwa wanawake kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wenye kutumia huduma za kibenki kutoka asilimia 66 mwaka 2017 hadi asilimia 80 mwaka 2023.
“Mafanikio haya ya ushirikishwaji wa kifedha kwa wanawake ni matokeo ya kuongezeka kwa utoaji wa namba ya vitambulisho vya taifa kwa wanawake na bidhaa za kifedha sasa zinafukiwa na wanawake”amesema.
Ameogeza kuwa Mustakabali wa Afrika unauwezekano mkubwa wakutokufikiwa ikiwa wanawake na wasichana wataachwa nyuma.
Kwa upande waziri ya maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalumu Dorothy Gwajima amesema kuna haja kubwa ya kuwekeza kwenye jinsia ili kuisaidia serikali kutotumia fedha nyingi kwenye mapambano ya jinsia badala yake fedha hizo zipelekwe kwenye mahitaji ya kijamii.
Amesema maswala ya ukatili wa kijinsia yanayofanywa kutokana na Mila na desturi yanarudisha nyuma maendeleo ya wanawake ambao wanamvhango mkubwa kwenye maendeleo ya sekta zote.
“Kwa kuacha hizi tabia kandamizi zitasaidia hizi fedha tunazotumia katika kupambana na ukatili zikaongezwa kwenye maendeleo na swala la ukatili si swala la Tanzania tu ni swala la bara zima la Afrika”
Aidha amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupiga hatua katika kuendeleza na kuwekeza kwenye maswala ya kijinsia kwani sasa hivi idadi kubwa ya viongozi nafasi ya mwanamke ipo na inafanya vizuri.
Naye,Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba amesema kuwekeza kwa wanawake ni kichocheo kikubwa cha uchumi katika nchi hivyo serikali itaendelea kuwawezesha na kutunga sera zitakazosimamia mopango na maendeleo endelevu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanda ya mashariki UN WOMEN Dkt. Maxime Houinato amesema mawaziri wa fedha wanahitajika ili kuangalia namna bora ya kuwawezesha wanawake.
Aidha Dkt. Houinato ametoa rai kwa serikali na sekta binafsi kuhakikisha mabinti wanapotoka chuo wasaidiwe kupata kazi ili kuepuka kuingia kwenye ukatili.