……………………..
Hatua inayochukuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Malikale nchini ya kufanya utambuzi na tathmini ya hali ya uhifadhi wa maeneo na Majengo yote ya Malikale katika mji Mkongwe wa Bagamoyo kwa lengo la kuandaa mpango wa usimamizi wa malikale hizo ambao umetajwa kuwa unakwenda kuifungua Bagamoyo zaidi Kiutalii.
Akizungumza na timu ya Wataalam wa Mambo ya Kale Wizara ya Maliasili na Utalii, waliofika ofisini kwake Wilayani Bagamoyo, Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Bi Sarah Ngwere amepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara hiyo na kuwa hatua hiyo inayoichukuwa itakuwa kichocheo kikubwa ongezeko la Watalii na kuwafanya waongeze siku zaidi za kutalii Bagamoyo.
Aidha Bi Ngwere, amesema Ofisi yake ipo tayari kutoa ushirikiano unaotakiwa ili kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa Mafanikio ili iweze kuongeza tija katika mapato ya Wilaya ya Bagamoyo na nchi kwa ujumla.
Naye Diwani wa Kata ya Dunda Mhe Amiri Mpwimbwi licha ya kupongeza jitihada za Serikali inazozichukuwa kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Wataalam hao kwa kuwa jitihada hizo ni Kwa maslai mapana ya Wanabagamoyo na Taifa kwa ujumla na kuwa itavutia Watalii wengi hasa wanaopitia Zanzibar kwa kuwa Bagamoyo ni rahisi kufikika kutoka Zanzibar.
Mhe. Mpwimbwi ameongeza kuwa changamoto ya utambuzi wa Mji mkongwe ndio unaorudisha nyuma mji wa Bagamoyo, hivyo hatua inayochukuliwa na Wizara itapelekea watu wengi kutambua mipaka sahihi ya Mji mkongwe hali itakayopelekea urahisi wa Uhifadhi urithi wa Malikale uliopo Bagamoyo.
Akielezea zoezi hiyo, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mambo ya Kale. Dkt. Emmuel Bwasiri, amesema nidhamira ya Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya Mji Mkongwe wa Bagamoyo kuwa kivutio kikubwa cha Utalii ili uchangie zaidi kwenye pato la Taifa na kuwainua kiuchumi wananchi wa Bagamoyo na waishio jirani.
Wizara ya Maliasili kupitia Idara ya Mambo ya Kale, inaendelea kutekeleza mkakati wa Kuorodhesha Malikale zikiwemo Majengo, Minara, Makaburi na maeneo ya Kihistoria nchini, hivyo imetuma timu ya wataam wa Malikale Wilayani Bagamoyo kuendelea na kazi hiyo.