Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamadi Rajabu akimsikiliza Mkuu wa kitengo Cha Habari Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo.
……………………..
Na Ali Issa Maelezo 14/11/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametangaza kulinunua goli moja kwa Shilingi Millioni moja kwa mchezo wa Fainali kati Uganda na Karume Boys ya Zanzibar utakaochezwa siku ya Alhamisi huko Uganda.
Tamko hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndugu Fatma Hamad Rajab wakati alipokuwa na mazungumzo na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Migombani.
Amesema Rais ametoa tamko hilo ili kuwapa hamasa wachezaji na wajue kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaridhishwa na jitihada zao na ipo pamoja nao.
Amesema Serikali kwa ujumla wameridhishwa na mchezo wanaocheza hasa pale inapoona wamefanikiwa kuwashinda wapizani wao kwakila wanapoingia kiwanjani.
“Mhe, Rais ameipongeza timu hiyo na Viongozi wake kwakufunzu kuingia fainali michuona ya CECAFA”alisema katibu Mkuu.
Hata hivyo, Dkt. Mwinyi aliigiza Wizara kuhakikisha kuwa mchezo huo unaoneshwa moja kwa moja ili Wazanzibari waishuhudie timu yao inavyopambana.
Mapema nae Rais wa Shirikisho la Michezo Zanzibar Suleiman Mahmuod Jabiri alisema kua mashindano ya Mabaraza ya Vyama vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA kwa wenye umri chini ya miaka 15 yaliaza rasmi mwaka jana lakini kwa upande wa Zanizibar ndio mara yake ya kwaza kushiriki mashindano hayo.
Aidha alisema kwa ujumla Shikisho la Michezo wanatoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuipa michezo nafasi kubwa na sasa Zanzibar ipo katika kiwango kizuri kimichezo.
Pia alishukuru Wizara na Viongozi wake kwa kujipanga vyema kuona michezo inaenda vizuri na Vijana wanapata nafasi kushirik katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Alisema Timu hiyo imecheza mechi nne na iliaza na Ruwanda ambapo Zanzibar ili shinda tatu bila, wakacheza mechi ya pili dhidi ya bingwa mtetezi Somalia na pia Zanzibar iliishinda nne bila na baadae walimalizia na ndugu zao Tanzania bara na ilishinda mbili bila.
Waliingia nusu fainali ambapo walicheza jana na Sudani ya Kusini na walifungana moja moja na kulazimika Matuta na Zanzibar ilishinda penanti zote nne zilizo wafanya kuingia fainali itakayo chezwa siku ya Alhamis.
Michezo Nasima Haji Chumu wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya CECAFA yanayoendelea Nchini Uganda ambapo Timu ya Zanzibar Karume Boys imeingia Fainali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.
PICHA NO-9762-Rais wa Shirikisho la Mpira Zanzibar ZFF Suleiman Mahmoud Jabir akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya CECAFA yanayoendelea Nchini Uganda ambapo Timu ya Zanzibar Karume Boys imeingia Fainali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.
PICHA NO-9800-Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamadi Rajabu akisisitiza jambo wakati alipokua akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya CECAFA yanayoendelea Nchini Uganda ambapo Timu ya Zanzibar Karume Boys imeingia Fainali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.
PICHA NO-9803-Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar ZFF Suleiman Mahmoud Jabir akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya CECAFA yanayoendelea Nchini Uganda ambapo Timu ya Zanzibar Karume Boys imeingia Fainali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.