Katibu wa NEC Saiasa, Itikadi na Mafunzo Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Paul Makonda amesema “Nafahamu ya kwamba zipo bodaboda zilizotumia fursa ya mpaka kufanya biashara za magendo hilo halipingiki na mimi ni msema ukweli lakini wapo Wananchi ambao wameendelea kufanya shughuli zao katika kusongesha maisha yao na hili sio la kupinga”
“Sasa Maelezo ya CCM na Mkuu wa Mkoa upo hapa Mhe. Mtanda upo hapa, na nimemsikia Mhe. Waitara anasema nimpigie simu Waziri wa Fedha, sasa hili swala wala sio la kupiga simu ni maelekezo tu ya Chama Cha Mapinduzi, kuanzia sasa leo tarehe 14 hadi ifikapo kesho tarehe 15 pikipiki zote zilizokamatwa Silali warudishiwe pikipiki zao na kama kuna mali zilizokamatwa watozwe kodi warudishiwe mali zao na kuanzia hapo utaratibu wa kisheria ufuate mkondo wake, wapeni fursa watu wafanye biashara kama ni bodaboda alipe kodi, ushuru achukue bidhaa auze, CCM Oyeee”
Wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Wananchi wa mjini Tarime Mkoani Mara , leo tarehe 14 Novemba, 2023.