Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa akizungumza wakati wa droo ya kutafuta washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) akisisitiza jambo wakati wa droo ya kampeni ya Kopa Tukubusti. Madhumuni ya kampeni Kopa Tukubusti ni kuwafaidisha wateja wa benki hiyo. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa (katikati) akimsikiliza kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru. Kulia ni afisa wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano wa kampuni ya Radian Limited Kundani Makimu.
………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Benki ya Letshego Faidika imesema inajisikia fahari kubwa kuwawezesha wateja wao kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti ambayo itamalizika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa wakati wa kuchezesha droo ya kampeni hiyo ambapo jumla ya washindi watano walipatikana.
Washindi hao ni Shaaban Ndunguru, Ndensari Kimaro, Jamal Mfinanga na Kiliani Chale ambao wameshinda fedha taslimu wakati Emmanuel Shibuga ameshinda pikipikii.
Washindi hao watano wanaungana na wengine 15 ambao wameshinda katika droo hiyo mpaka sasa.
Bw Nalingigwa amesema kuwa kampeni hiyo inamtaka mteja wao kukopa fedha taslimu na kuingia kwenye droo ambayo mshindi atapata asilimia 50 zaidi ya kiasi alichokopa.
Aliwapongeza washindi hao kwa kujipatia fedha hizo ambazo uwekwa kwenye akaunti ya mshindi moja kwa moja.
Bw Nalingigwa alisema kuwa kampeni hiyo inazidi kushika kasi na kuwaomba wateja wao kuchangamkia mikopo yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kuweza kusaidia kugharimia mahitaji mbalimbali.
Benki hoyo imetenga kiasi cha Sh50 billion kwa ajili ya kuwazawadia wateja wao kupitia kampeni hiyo.
“Tumeweka jumla ya Sh50 biliioni kwa ajili ya kukopesha wateja wetu. Mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya Kopa Tukubusti. Lengo hapa ni kubadili maisha ya wateja wetu. Kwa mfano, mteja anaweza kukopa mpaka kiasi cha Sh milioni 150 ambapo akishinda kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti, atazawadiwa Sh milioni 75,” alisema Bw. Nalingigwa.
Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo Kubashiri, Pendo Mfuru aliwaomba Watanzania kuchangamkia fursa hiyo ili kuweza kutatua mambo mbalimbali.