WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Professa Adolf Mkenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la kusherehekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Cha Afya na Tiba Kishiriki Muhimbili(MUHAS).
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Appolnary Kamuhabwa alisema hayo jana Jijini Dar es Salaam kuwa kongamano litafanyika Alhamis ya Novemba 16, wiki hii Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu huyo wa Chuo alisema kuwa kongamano hilo litawa leta pamoja takribani washiriki 300 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wasomi wa vyuo vikuu vya tiba,wahadhiri,wahitimu wa Chuo hicho, wazazi, washiriki kutoka sekta binafsi,wadau wa Maendeleo na viongozi kutoka serikalini.
Alisema kongamano hilo litaakuwa mada mbalimbali kuonyesha mahali chuo kilipotoka,kilipo na kinapokwenda na kuongeza kuwa litaambatana pia na maonyesho ya ubunifu wa kisayansi.
“katika miaka hii sitini ya kuwepo kwa Chuo chetu, tumefanikiwa kuongeza udahili na kufikia wanafunzi 4000 kwa mwaka kutoka wanafunzi 10 kilipoanzishwa na kozi kufikia 101 ambapo 81 ni za ngazi ua udhamili na udhamivu,”alisema porfesa kamuhabwa.
Professa Kamuhabwa aliongeza kusema kuwa Chuo hicho kimeandaa pia matembezi ya hisani yatakayofanyika novemba 18 ,jumamosi hii, sambamba na upimaji wa afya bure wa magonjwa kama kisukari na shinikizo la juu la moyo.