Mkuu wa Mkoa wa Mjni Magharibi Mhe.Idriss Kitwana Mustafa akizungumza wakati akifungua kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja
Kamisaa wa Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 Tanzania Zanzibar Balozi Mohammed Haji Hamza akizungumza katika kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Salum Kassim Ali akizungumza wakati wa kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja.
Baadhi ya Masheha na Madiwani wakifuatilia kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja
Ofisa kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Nassir Hamad Salum akiwasilisha baadhi ya matokeo ya sensa kwa kutumia ramani kwa Mkoa wa Kusini Pemba Wakati wa kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja
Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed Mussa akichangia mada Wakati wa kikao chausambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Hamida Khamis Mussa akichangia mada Wakati wa kikao cha usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja.
Sheha wa Shehia ya Urusi Wadi ya Jang’ombe Yussuf Juma Mtumwa akichangia mada wakati wa kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya iashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja.
Diwani wa wadi ya Pangawe Mwan-jaha Nahoda Maulid akichangia mada wakati wa kikao cha usambazaji wa matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja.
Diwani Manispaa ya Mjini Amour Mmanga akichangia mada Wakati wa kikao cha usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya viashiria vya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 ngazi ya Mkoa huko Polisi Ziwani Mjini Unguja
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Na Fauzia Mussa , Maelezo
Mkoa wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Watendaji wa ngazi za Wadi na Shehia kuyatumia matokeo ya Sensa ya watu na makaazi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.
Akizungumza na Masheha na Madiwani wakati akifungua kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya viashiria vya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 huko Polisi Ziwani Mkuu huyo alisema endapo matokeo hayo yatatumika vizuri jamii itaweza kupanga mipango ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
Aidha alisema Takwimu ya idadi ya watu itasaidia katika kuweka rasilimali ambazo zinatumika katika kukuza Uchumi wa Taifa na kupatikana kwa huduma za jamii kwa urahisi hivyo aliwataka Viongozi hao kutumia matokeo hayo katika ugawaji wa rasilimali kwa lengo la kuleta maendeleo Nchini.
Sambamba na hayo alitoa wito kwa Masheha na Madiwani kuwa Mstari wa mbele katika kufikisha taarifa hizo kwa jamii ili kusaidia Serikali katika kutoa huduma sahihi kwa wananchi.
Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Salum Kassim Ali alisema Matokeo ya Sensa ni Muhimu kwani yanasaidia kupanga, kusimamia pamoja na kubadilisha maisha ya Wananchi.
“Takwimu ya idadi ya watu itasaidia katika kusimamia mchakato wa kutoa huduma kwa Wananchi kwa lengo la kupata Maendeleo katika Nchi” alisema Mtakwimu huyo
Alisema taarifa zinazotolewa na Wananchi ndizo zinazoiwezesha Serikali kubadilisha hali za Wananchi kwa kuwaletea Maendelo,hivyo kuna kila sababu ya Wananchi kupatiwa uwelewa wa umuhimu wa kutoa taarifa sahihi ili kueka mipango madhubuti katika upatikanaji wa huduma ikiwemo huduma za Afya.
Kwa upande wake kamisaa wa Sensa anaefanyia kazi zake Zanzibar Balozi Hamza Haji Hamza amesema kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mawaka 2022 imeonesha kuwa Mkoa wa Mjini Magharibi una idadi kubwa ya wakaazi ukilinganisha na mikoa mingine ya Zanzibar.
Hata hivyo aliwapongeza Masheha kwa kufanikisha kazi ya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 kuanzia matayarisho hadi kupatikana kwa matokeo mazuri.
Katika kikao hicho mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo matokeo muhimu ya baadhi ya Viashiria vya kiuchumi ,Kijamii na mazingira vitokananvyo na sensa ya watu na makaazi