Wananchi wa Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Busega wameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezw na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa.
Hayo yamejidhiirisha wakati ambapo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda aliposimama kuzungumza na Wananchi wa Wilayani Busega ambapo waliwakilishwa na Mbunge wao wa Busega Mhe. Saimon Songe aliyeeleza kwa ufasaha namna fedha nyingi zilivyoletwa na Serikali ya Mama Samia kwa utelelezaji wa miradi
Mbunge Simon Songe amesema kissing cha shilingi Bilioni 400 zimeletwa kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo cha Veta.
Shilingi Bilioni 2.287 kwa ajili ya miradi ya barabara kila kata ambapo miradi yote hiyo utekelezaji wake unaendelea.
Mbunge huyo ameongeza kuwa Serikali imejenga Vituo vya Afya 4 kwa wakati mmoja vilivyogharimu jumla ya Bilioni 2.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt. Yahya Nawanda akielezea zaidi ameainisha fedha mbalimbali kwa ujumla wake katika miradi mbalimbali kama ifuatavyo;
Amesema zaidi ya shilingi Bilioni 444 zimepokelewa mkoani Simiyu kwa ajili ya Mradi wa Maji Busega – Bariadi – Maswa hadi Meatua Huku zaidi ya shilingi Bilioni 60 zikipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme ambacho kinatarajiwa kujengwa Bariadi katika njia kuu ya kuunganisha na Shinyanga.
Vilevile Mhe. Dkt. Nawanda amebainisha kuwa tayari wameshaandika barua kuomba fedha shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko, shilingi Bilioni 8 na Stendi kuu ya Busega imeombwa shilingi 2.6) ambapo amemuomna Katibu Mwenezi Ndugu Paul Makonda kusaidia kusukuma jambo hilo kwa Mh. Rais Dkt. Samia
Akizungumza na Wananchi hao, Ndugu Paul Makonda amesema Rais Samia kwa kazi hii kubwa anayoendelea kuifanya maana yake ameweka deni kanda ya ziwa kwani ridhaa ya kuongoza 2020/25 matokeo yake chanya yanaonekana sasa ni kumuombea kwa Mungu ilikusudi 2025 katika uchaguzi Mkuu nasi wana Kanda ya ziwa tulipe deni.
Aidha, amemhakikishia Mkuu wa Mkoa Simiyu kwamba Chama kitaweka msukumo mkubwa katika kuhakikisha fedha walizoomba zinapatikana kwa haraka ili miradi hiyo ianze na kukamilika kwa wakati