Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC),Itikadi,Uenezi na Mafunzo Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Mwanza akiwa katika ziara yaikoa ya Kamda ya Ziwa.
……………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC),Itikadi,Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia barabara mbili za kutoka Mwanza mjini hadi usagara na Mwanza mjini hadi Igoma ziingie kwenye mpango na kufanyiwa usanifu ili azitafutie pesa ili zijengwe barabara nne katikati ya Jiji la Mwanza.
Ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea Mikoa ya Kanda ya ziwa.
Makonda amesema kuwa barabara inayotoka Igoma kwenda Kishiri mkataba wake utasainiwa Novemba 20 Mwaka huu ili ujenzi uanze kutekelezwa kwa kiwango cha rami.
Katika hatua nyingine Makonda ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza ni wa pili kwa kuwa na abiria wengi wanaotumia usafiri wa ndege hivyo uwanja wa ndege wa Mwanza haupasi kuwa hivyo ulivyo kwani kunausumbufu mkubwa ukiwemo wa watu kusumbuka kuchukua mzigo.
Kutokana na Changamoto hiyo Makonda alimpigia simu Waziri wa Uchukuzi Mhe.Makame Mbarawa ili kupata majibu ya lini uwanja huo utakamilika.
Akitoa majibu kwa njia ya simu Waziri huyo alisema mkataba wa ukarabati wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza utasainiwa baada ya wiki mbili baada ya hapo mkandarasi atapewa miezi 10 na itakapofika Novemba 2024 jengo la abiria litakuwa kimekamikika kwa asilimia 100.