Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hassan Khamis Hafidh akizungumza na wadau wa saikojia wakati akifungua Jukwaa la siku ya saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar ZU na kufanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Mkalimani wa lugha za Alama akiwasaidia uelewa wenye mahitaji maalum katika Jukwaa la siku ya saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar ZU na kufanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja
Msanii wa tungo za mashairi Kassim Yussuf akisoma utenzi wenye maudhui ya umuhimu wa taaluma ya tiba ya saikolojia na Ushauari nasihi katika Jukwaa la siku ya Saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar ZU na kufanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baaadhi ya wadau wa Saikolojia wakifuatilia hafla ya Jukwaa la siku ya Saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar ZU na kufanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
…….
Na Imani Mtumwa Maelezo Zanzibar 12/11/2023
Wanasaikolojia wametakiwa kufanya uchunguzi wakati wanapofanya kazi zao ili kuleta maendeleo katika jamii kwani taaluma hiyo inasababisha kupatikana ufumbuzi wa haraka.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Afya Mhe Hassan Khamis Hafidh wakati akizindua jukwaa la siku ya Saikolojia Ukumbi wa Idrisa Abdulwaki Kikwajuni Zanzibar.
Aidha amefahamisha kuwa taaluma hiyo ni muhimu kupatiwa Vijana kwani elimu ya Saikolojia inahitajika katika harakati mbali mbali za maendeleo.
Hata hivyo amesema matibabu ya Saikolojia nimuhimu kwa Wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi sugu kama vile maradhi ya moyo, saratani hivyo wagonjwa hao wanahitaji tiba ya Saikolojia ili kuweza kukubaliana na hali hiyo.
Nae Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdallah amewapongeza Jumumuia ya Wanafunzi Saikolojia (ZUPCSA) Kwa kuandaa Jukwaa hilo linalosaidia kutoa Elimu kwa jamii.
pamoja na hayo katibu huyo liwaomba wadau wa Saikolojia kuunga mkono juhud za ZUPCSA za kuendeleza kufanya Jukwaa hilo kila Mwaka.
Akisoma Risala kwaniaba ya ZUPCSA Mwekiti wa jumuia hiyo Ramadhan Muhammed amesema Taaluma hiyo bado ni mpya hivyo wanaendelea kutota Elimu kwa jamii kuweza kufahamu umuhimu wa Taauma hiyo.
Hata hivyo waliiomba Serekali kuanzisha chombo au bodi maalum itakayosimamia wahitimu wa taaluma hiyo kuweza kupatiwa leseni na kutambulika kama zilivyo taaluma nyengine nchini.
Jukwaa la siku ya Saikolojia ni latatu kufanyika tangu kuanzishwa taluuma hiyo katika Chuo Kikuu cha Zanzibar ambapo Mwaka huu jukwaa hilo limebeba ujumbe “Afya ya Akili na Tiba ya Saikolojia ni haki kuu ya Binaaadamu.”