Na Ashrack Miraji – Same kilimanjaro
Wanawake katika maeneo mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani na serikali yake kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta Maendeleo kwenye jamii na kuboresha upatikanaji wa huduma.
Wito huo umetolewa na do wa Viti maalum wilaya ya Some mkoani Kilimanjaro Mhe. Zaina Mghamba wakati akizungumza na wakazi wa tarafa ya Chome Suji kwenye mkutano na wanawake wote wa tarafa hiyo maalum kujadili Uhai wa Chama cha Mapinduzi na jumuiya zake nakujadili pia namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto.
“Niwaombe Wanawake wenzangu tuwalinde watoto wetu pindi watokapo mashuleni dhidi ya watu wenye tabia zisizo faa kuhakikisha wanakuwa Salama pia lazima kukilinda chama chetu cha Mapinduzi pamoja na kuendelea kumsemea vyema kwa Wananchi Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa maendeleo makubwa aliyotufanyia hasa kwenye wilaya yetu”. Amesema Mhe.Zaina Mghamba.
Pamoja na Hayo amewata Wanawake kuacha tabia ya kuwa tegemezi kwa wenza wao lazima bdala yake kujikita kwenye shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo ujasiriamali hata kutengeneza Sabuni za Maji na Batiki Lengo ni kutomeza umaskini na kuleta Maendeleo kwa pamoja.