Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza jana na Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kuwandaa Majaji ya Nchini Kazakhstan wakati wa ujumbe aliouongoza ulipokwenda kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo wanavyotoa mafunzo.
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Majaji ya Kazakhstan iliyopo chini ya Mahakama ya Upeo Baimoldina Zauresh Hamitovna (katikati) akitoa maelezo jana kwa ujumbe wa Mahakama ya Tanzania uliokwenda kujifunza jinsi wanavyowaandaa Majaji kabla ya kuteuliwa.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania Mhe. Dkt. Angelo Rumisha (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanunizi kwa Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kuwaandaa Majaji ya Kazakhstan wakati wa ziara ya mafunzo katika Taasisi hiyo jana.
Ujumbe wa Mahakama ya Tanzania(kulia) ukiwa na Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Majaji ya Kazakhstan (kushoto) wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu jana juu mafunzo kwa Majaji watarajiwa na waliopo madarakani.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kuwaandaa Majaji cha Nchini Kazakhstan Baimoldina Zauresh Hamitovna ( kulia) mara baada ya mkutano wa pande mbili jana wa kubadilisha uzoefu juu ya kuwaendeleza Majaji na kuwaandaa wapya.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati), akiwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresha cha Mahakama ya Tanzania Mhe. Dkt. Angelo Rumisha(.wa saba kutoka kulia ) , Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya kuwaandaa Majaji ya Kazakhstan iliyopo chini ya Mahakama ya Upeo Baimoldina Zauresh Hamitovna (pembeni Prof. Ole Gabriel ) , Ujumbe wa Mahakama ya Tanzania na Uongozi wa Taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano jana wa pande wa kubadilisha uzoefu kuhusu maandalizi ya Majaji na mafunzo wakiwa kazini.
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kuwaandaa Majaji ya Kazakhstan Baimoldina Zauresh Hamitovna( wa kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa ujumbe wa Mahakama ya Tanzania uliotembelea Taasisi hiyo jana kwa lengo ya kujifunza na kubadlishana uzoefu.
……….
NA Tiganya Vincent-Astana -Kazakhstan
Taasisi ya Mafunzo kwa ajili ya kuwaanda Majaji ya nchini Kazakhstan imesema iko tayari kushiriana na Chuo cha Uongozui wa Mahakama Lushoto nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuimarisha utendaji na kuwaendeleza Maafisa hao wa Mahakama.
Hatua hiyo imefikiwa jana tarehe 10 Novemba 2023 katika mji Mkuu wa Kazakhstan wa Astana wakati mkutano kati ya ujumbe wa Mahakama ya Tanzania uliongozwa na Mtendaji Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel pamoja na ule wa Taasisi ya Majaji ya Mahakama ya Upeo ya Kazakhstan.
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Majaji ya Kazakhstan iliyopo chini ya Mahakama ya Upeo Baimoldina Zauresh Hamitovna alisema kuwa wao wako tayari kuingia makubaliano na Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto cha Tanzania kwa lengo la kubalishana uzoefu kitaaluma na kuboresha sekta ya utoaji haki kwa pande zote.
Alisema kwa muundo wao kabla ya mtu kuwa Jaji anatakiwa kushiriki mafunzo ya Shahada ya Uzamili(Master Degree) ya Sheria katika Taasisi hiyo na ilia pate udahili anapaswa kuwa miaka 28 kuendelea, Stashaha(Diploma) katika fani ya Sheria na uzoefu usiopungua miaka mitano.
Zauresh aliongeza kuwa nchini Kazakhstan kuna njia mbili za kuwa Jaji ,ikiwa ya Kwanza lazima mtu awe amesoma Stashahada(Diploma) ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Nchi hiyo na ya pili ni lazima mtu asome katika Taasisi ya Mafunzo kwa ajili ya kuwaanda Majaji na kufaulu mitihani yote.
Alisema mtu anayepitia katika Taasisi ya Mafunzo ya kuwaanda Majaji anakuwa na nafasi kubwa ya kufaulu wakati wa ushindani wa kuwatafuta watu wanaostahili kuteuliwa kuwa Majaji nchini humo.
Awali Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel aliuomba uongozi wa Taasisi hiyo kuangalia uwezo wa kuingia makubaliano ya kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto nchini Tanzania katika kubadiliana uzoefu wa kuwaendeleza Maafisa Mahakama na Watumishi wengine.
Alisema kuwa Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto kimekuwa na utaratibu wa kuwapa mafunzo elekezi, Majaji, Mahakimu na Watumishi wengi wasio Maafisa wa Mahakama kabla ya kuanza majukumu yao mapya , jambo ambalo limesaidia kufanyakazi kwa ufanisi ndani ya Mahakama ya Tanzania.
Prof. Ole Gabriel alisema wakikubaliana wanaweza kuandaa Programu ambazo zinaweza kufundishwa katika pande mbili kama sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujngeana uwezo kwa watumishi na Maafisa wa Mahakama waliopo kazini na wale walioteuliwa kuingia kazini.
Alisema endapo watakubaliana , uongozi wa Mahakama ya Tanzania utahakikisha unasimamia makubaliano yaliyofiukiwa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Angelo Rumisha alisema alisema kwa Tanzania Majaji wanaandaliwa kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali kwa kupata Shahada ya Sheria na kupita katika Shule Kuu ya Sheria na wanapoteliwa wanapata mafunzo elekezi katika Chuo cha Uongozi Lushoto.