Na Sophia Kingimali
Rais wa Chemba ya Biashara,Viwanda na KilimoTCCIA Vicent Minja amesema uongozi mpya uliochaguliwa ukiongozwa na yeye wameweka mikakati ya kuhakikisha sekta binafsi inashirikiana na serikali katika kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi.
Hayo ameyasema leo Novemba 10,2023 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotangaza bodi mpya.
Amesema bodi hiyo imejipanga kuhakikisha inaimarisha ushirikiano wa dhati na wanachama,wafanyabiashara na wadau ili kuhakikisha sauti zao zinasikika kwa kila hatua wanayoichukia.
“Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali na wadau wengine ili kuhakikisha biashara,viwanda na kilimo vinapiga hatua mbele na tunaweka mikakati imara ya kuvutia uwekezaji,kutoa mafunzo na kusaidia miradi inayochangia ukuaji wa sekta hizi”amesema Minja.
Ameongeza kuwa wataendeleza ubunifu na teknolojia katika utoaji wa vyeti vya uasili(Certificate of Origin) ambapo wanahimiza matumizi ya teknolojia na ubunifu katika biashara,viwanda na kilimo.
Aidha Minja ameongeza kuwa uongozi huo umejipanga kuimarisha ushirikiano na serikali,taasisi ,balozi, wadau wa maendeleo ba chemba za kimataifa lengo likiwa kufanisha kufikia maendeleo endelevu yaliyokuwepo na yanayoendelea kuchanua katika chemba hiyo.
Amesema kwa kutumia uzoefu wao wa miaka 35 katika huduma na uongozi wa sekta binafsi nchini wataendelea kusimamia kusimamia mabalaza ya biashara.
Kwa upande wake makamu wa Rais TCCIA anaeshughulikia kilimo Swallah Swallah amesema zaidi wa watanzania asilimia 90 wapo kwenye sekta ya kilimo hivyo wamejipanga kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa muhimili muhimu katika uchumi wa nchi.
Nae,Makamu wa Rais anaeshughulikia biashara Boniface Ndego amesema wamejipanga kuchochea mageuzi makubwa kwenye masoko ili kujenga uchumi wa taifa.
Aidha ameongeza kuwa wataunganisha sekta binafsi na kuchochea ujenzi wa makampuni makubwa ili kutanua wigo wa biashara lakini kuwezesha mitaji ya kuanzisha biashara mpya na kuendeleza biashara.