Dodoma, Tanzania
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM), Prof. Razack Bakari amepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza teknolojia ya akili bandia nchini.
Pia, ameipongeza timu iliyofanikisha uandishi wa andiko bora la mradi wa kutengeneza Teknolojia rafiki itakayosaidia kutatua matatatizo ya afya ya akili na kufadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Akizungumza jana katika uzinduzi wa mradi huo, Profesa Razack alisema mradi huo ni bora na utasaidiana katika kukabiliana na changamoto za afya ya akili nchini.
“Ninatambua matumizi ya akili bandia yanasaidia Afrika na Dunia kwa ujumla kuakisi malengo 17 endelevu (SDG), teknolojia hii ikitumika ipasavyo zinasaidia kutoa majibu ya changamoto katika sekta ya afya, kilimo, utunzaji wa mazingira na uchumi wa kidigitali ” alisema Prof. Razack
” Ninatambua kulingana na Takwimu za WHO tatizo hili ni kubwa na inakadiriwa kuwa watu takribani mil 970 , kati ya mtu 1 mpaka 100 vifo vyao vinatokana na kujiua (suicide) huku kukiwa na asilimia 50 ya vifo vilivyotokea duniani kwa kipindi cha miongo 5 na twakimu duniani zinaonesha kati ya mtu 1 – 4 wanasumbuliwa na tatizo la afya ya akili na asilimia 60 hawafiki vituo vya afya kupatiwa matibabu ikiwemo kizazi cha sasa cha Tanzania kinatwakimu Sawa kama zinavyoiathiri dunia ya sasa kwa sababu ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia” alisisitiza Prof. Razack.
Akifafanua lengo la mradi wa kutengeneza Teknolojia rafiki itakayosaidia kutatua matatatizo ya afya ya akili, mtafiti Dkt. Jabhera Matogoro alisema
” Mradi huu unafadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), na lengo lake kubwa ni kutengeneza Teknolojia itakayosaidia kutatua matatatizo ya afya ya akili” alisema Dkt. Matogoro
Aliongeza kuwa, mradi huu tunashirikiana na wenzetu wa chuo kikuu cha Nelson Mandela, Chuo kikuu cha dodoma na hospital ya Taifa ya afya ya akili ya mirembe na utakuja na majibu yatakayosaidia kutatua changamoto hiyo ” aliongeza dr matogoro
” Mradi huu una malengo makuu matatu ikiwemo utatengeneza kanzidata (database) kuwezesha utengenezaji wa mifumo ‘software’ zitakazojibu changamoto zinazokabili wananchi na lengo la Tatu ni kuweka mfumo ule kuanza kutumika maeneo mbalimbali ” alisisitiza Dkt. Matogoro
Kwa upande wake, Dkt. Godwin Mwisomba alisema mradi huu unaofadhiliwa na Serikali kupitia COSTECH utsaidia kupata utambuzi wa haraka na kutoa tiba mapema kwa hatua za awali kabla haijafika kuwa tatizo hususani kwa watumiaji wa mitandao na simu, itasaidia kutoa huduma ya Kwanza na msaada wa kisaikolojia kwa watanzania wote.
“Tunaona ni suala zuri na jema , tunatoa rao kama wadau wasaidie kusupport ili mradi huu uweze kuwa mkubwa na uhusishe watanzania wote, tunaamini kila kaya inayomtumiaji wa simu na itaifikia kila kaya na tunaweza kuingilia mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa” alisisitiza dkt. Mwisomba.
Naye, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Taaluma, Utafiti na Ushauri kwa Umma, Prof. Razack alisema uzinduzi wa mradi utasaidia kugundua
Mradi wa matumizi ya Teknolojia hii mpya utasaidia kupata takwimu muhimu sahihi za magonjwa tofauti ya afya ya akili
Alihitimisha kuwa, teknolojia hii itasaidia kutoa tiba na ufanyaji tafiti mbalimbali na kikubwa tunashukuru Serikali kutukutanisha kwa Taasisi za Elimu ya Juu zinashirikiana na Taasisi za tiba na kutoa matokeo yanayotumika kutatua matatatizo yaliyopo katika jamii na kuhamasisha watafiti wengine kuendelea kujitokeza ili kupata mwamko mkubwa.