Na Sophia Kingimali
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Oval Technologies Limited inayojihusisha na utengenezaji wa mifumo ya kompyuta Ally Salum ametoa rai kwa kampuni changa (Startups)kushiriki kwenye maonesho ya teknolojia ili kujifunza kwa wengine na kupata fursa.
Hayo ameyasema Novemba 9,2023 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Teknolojia za kifedha kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere JNICC.
Amesema nchi imepiga hatua kubwa katika ukuaji wa kidigitali hivyo ni vyema kampuni za kiteknolojia kushirikiana ili kuhakikisha adhima ya serikali inatimia.
“Sisi ni mara yetu ya kwanza tangu kuanzishwa kwa kampuni yetu 2018 kushiriki maonesho haya lakini tumepata fursa ya kujifunza kwa wengine lakini pia fursa mbalimbali hivyo tutaendelea kushiriki maonesho haya kila mwaka
Aidha Salum ameongeza kuwa kupitia mkutano huo wameweza kubadilishana mawazo na kampuni nyingi lakini pia wametanua wigo wa biashara yao.
Akizungumzia kampuni amesema kupitia mifumo wanayoitengeneza wameweza kuwa na mfumo unaoweza kusimamia vikundi vya kijasiliamali na miradi ya kikundi.
Ameongeza kuwa pia wanamfumo wakuweza kusimamia makampuni katika uendeshaji wa idara zake lakini pia usalama mahara pa kazi.
“Mfumo huu ambao tunao unasaidia kusimamia miradi unaweza kujua mradi unaanza lini na unaisha lini fedha kiasi gani, rasilimali watu fedha na mali zote mfumo unasaidia kila kitu”
Sambamba na hayo pia wametengeneza mfumo kwa ajili ya Wafanyabiashara unaofahamika kama smart mauzo ambao unawasaidia kufuatilia mwenendo wa biashara zao.