Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Y9 Microfinance Fredrick Moses Mtui , akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Eva Mbena kutoka Songea mshindi wa droo ya nne ya pakua app ya Y9 kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kifedha kama kununua Umeme, muda wa maongezi na huduma nyingine za kifedha kulia ni Meneja wa Masoko wa Taasisi hiyo Sophia Mang’enya Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za Y9 zilizopo Masaki jijini Dar wa Salaam.
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Y9 Microfinance Fredrick Moses Mtui , akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Iddy Kiluvia kutoka Njombe mshindi wa droo ya nne ya pakua app ya Y9 kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kifedha kama kununua Umeme, muda wa maongezi na huduma nyingine za kifedha Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za Y9 zilizopo Masaki jijini Dar wa Salaam.
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Y9 Microfinance Fredrick Moses Mtui akiazungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi wa droo ya nne ya pakua app ya Y9 katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Mshindi wa Droo ya nne ya pakua app ya Y9 Eva Mbena kutoka Songea .
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Y9 Microfinance Fredrick Moses Mtui , akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Iddy Kiluvia kutoka Njombe mshindi wa droo ya nne ya pakua app ya Y9 kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kifedha kama kununua Umeme, muda wa maongezi na huduma nyingine za kifedha Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za Y9 zilizopo Masaki jijini Dar wa Salaam.
……………………………
Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imewakabidhi zawadi zao za pikipiki Iddy Kiluvia kutoka Njombe na Eva Mbena kutoka Songea baada ya kuibuka washindi katika droo ya nne ya kampeni ya pakua app ya Y9 Microfinance na kupata huduma tatu ambazo ni kopo wa fedha taslimu, kopo wa fedha ya kununua umeme na mkopo wa fedha ya kununua muda wa maongezi.
Zawadi hizo zimetolewa leo Novemba 9, 2023 ji9jini Dar es salaam wakati ilipochezeshwa droo ya sita ya kampeni ya pakua app ya Y9 Microfinance inayochezeshwa kila siku ya alhamisi na kutoa washindi wa Pikipiki Simu hku kukiwa na droo kubwa ambayo itafanyika na kutoa mshindi wa gari Toyota IST.
Kiluvia kutoka Njombe na Eva Mbena kutoka Songea walikabidhiwa zawadi zao na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Fredrick Mtui ambaye ametoa rai kwa watanzania hasa wajasiriamali wadogo kukopa na kulipa kwa wakati ili kuendeleza biashara zao lakini pia kuingia kwenye droo ya kushinda pikipiki,simu na gari.
Fredrick Mtui amesema Y9 Microfinance inatambua na kuthamini jitihada za wajasiliamali hivyo imeongeza muda wa kurejesha mkopo kutoka siku tatu hadi siku tisa kutokana na kiwango unachokopa.
“Leo tumekutana kuwapongeza washindi wetu wa pikipiki na simu na kuchezesha droo ya sita ambao wiki ijayo tutakabidhi simu ya sita na pikipiki ya sita kwa hiyo watanzania kazi ni kwenu kupakua Application ya Y9 ili kuweza kukopa na kurejesha kisha kuingia kwenye droo tumebaki na simu mbili na pikipiki mbili lakini droo kubwa kabisa itatoka gari aina ya IST”amesema Mtui
Ameongeza kuwa awali walikua wanatoa mkopo wa shilingi 2000 mpaka 100000 lakini sasa wanatoa kuanzia 2000 mpaka 300000(laki tatu).
“Tupo kwa ajili ya kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo wadogo wapate mkopo wa haraka haraka ili wapate kuboresha biashara zao”amesema
Kwa upande wao washindi hao iddi Kejo kutoka Njombe na Mdeme kutoka Songea ambao wameshinda pikipiki wametoa rai kwa wananchi kupakua app hiyo na kuanza kukopa ili waweze kushinda na kubusti vipato vyao kwani droo hiyo ni ya kweli na haina upendeleo.