…,…..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Serikali Kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji(UNCDF) wameandaa mwogozo wa Kitaifa wa uanzishwaji na usimamizi wa Kampuni mahususi za kuendesha na kusimamia miradi ya vitega uchumi Halmashauri zote Nchini(SPV).
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku nne kwa wakufunzi wa wakufunzi takribani 20 kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika kusimamia miradi hiyo ya kitega uchumi iliyoanzishwa na miradi mipya inayoanzishwa.
Balandya amesema kuwa serikali zinapata changamoto ya uendeshaji na usimamizi wa miradi ya kiuchumi kuingiliwa kisiasa, uzoefu mdogo wa watumishi, kutoeleweka taratibu za uendeshaji wa miradi mapungufu katika usimamizi wa fedha na mifumo ya utoaji wa taarifa.
“Changamoto hizi ni miongoni mwa sababu zinazosababisha kutofikiwa Kwa malengo ya uanzishaji wa Miradi/ vitega uchumi husika” Alisema Balandya.
Ameeleza kuwa ili kufika malengo ya kuanzishwa Kwa miradi ya vitega uchumi vya Halmashauri imeonekana kuwa utaratibu wa kusimamia miradi Kwa kutumia makampuni mahususi(SPV).
“Uzoefu unaonesha kwamba kwa sasa miradi ambayo inatekelezwa Kwa utaratibu wa SPV imekuwa ikiendeshwa kwa ufanisi kuendana na malengo ya kuanzishwa kwake ikilinganishwa na miradi inayosimamiwa na mamlaka za serikali za mitaa zenyewe” Alisema Balandya.
Balandya ameeleza kuwa kuwepo kwa muundo mzuri wa Kampuni za kusimamia na kuendesha miradi katika mfumo wa Kampuni Mahususi kuwa ni miongoni mwa suluhisho la kukabiliana na changamoto za kuwezesha utekelezaji wa miradi husika katika kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
“Ili kuimalisha uwezo wa kitaalamu kwa mamlaka za Serikali za mitaa katika kuanzishwa na kusimamia miradi ya kimkatakati ya kuongeza mapato serikali imeona ni muhimu kuweka mwogozo wa uanzishwaji na usimamizi wa Kampuni mahususi” Alisema Balandya.
Kwa upande wake Afisa uwekezaji UNCDF Stella Lyatuu ameeleza kuwa serikali imeandaa mwogozo utakaowasidia kwenye Halmashauri kuweza kuendesha, kuanzisha na kusimamia miradi ya kimkakati inayozalisha na kipato Kwa njia ya kutumia Kampuni mahususi.
Stella ameeleza kuwa Miradi hiyo itawawezesha kuingiza kipato cha kujiendesha wenyewe na kuacha kutegemea kutoka serikalini na kuwasaidia namna ya kuendesha miradi kiufanisi na kutekeleza kitaalamu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi uratibu shughuli za serikali kwenye Mikoa Johnson Nyingi,ameeleza kuwa serikali kuandaa mwogozo huo utasaidia Halmashauri kuwa na uwezo wa kuzalisha mapato .
“Zitakapozalisha mapato zitawezesha kutoa huduma za kijamii ikiwemo huduma za afya, maji,elimu na kuwekeza maeneo mengine kulingana na fursa zao” Alisema Nyingi.