Na Sophia Kingimali
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) imesitisha leseni kwa mabasi 36 ambayo yalikuwa yakifanya safari za usiku kutokana na kuchezea mfumo wa kufatilia mwenendo wa Magari VTC na mwendokasi.
Ambapo kampuni zilizoongoza kuchezea mfumo wa VTS na mwendokasi ni pamoja na
Kampuni ya Capricorn, ambapo jumla ya mabasi tisa yalifugiwa na Abood bus service mabasi mawili, Dar express mabasi mawili, huku Kampuni 23 za mabasi zikifugiwa mojamoja
Mbali na hilo pia amesema LATRA imewafungia madereva 10 kutokana na kuchezea mfumo wa kufatilia mwenendo wa Magari VTC huku madereva 666 wakiandikiwa faini Kwa makosa ya mwendokasi na 32 wakifikishwa mahakamani, na 50 wakipewa onyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam novemba 9,2023 Mkurugenzi Mkuu LATRA, CPA Habibu Suluo wakati akitoa tathimini ya safari za mabasi kwa ratiba ya usiku saa 24 kwa mwezi mmoja toka Octoba 5 hadi Novemba 6 mwaka huu .
Amesema Novemba 6,2023 LATRA ilitoa ratiba za usiku kwa mabasi 246 kwa Kampuni wasafirishaji 46 kwa jumla ya njia 26 zinazoanzia Jijini Dar es salaam.
CPA Suluo amesema katika kufatilia mwenendo wa utoaji huduma kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo mfumo wa VTS, ratiba za mabasi, ukaguzi wa maeneo mbalimbali ilibaini baadhi ya wasafirishaji kuchezea mfumo wa VTS na kwenda mwendokasi unaotakiwa kisheria zaidi ikiwemo taarifa za abiria kutokuzigatiwa ipasavyo na kutokuacha orodha ya abiria katika vituo vya kuanzia safari.
“Kati ya madereva 246 madereva 110 sawa asilimia 44 awatumii mfumo wa utambuzi wa dereva ambapo kati ya mabasi 246 mabasi 197 sawa na asilimia 80 yanaenda mwendokasi kati ya kilometa 86-89 Kwa saa 09 asilimia wanaendesha mwendokasi kati ya kilometa 90 _103 Kwa saa”amesema Suluo
Amesema kuwa katika kuendana na azma ya Serikali ya kuruhusu utoaji huduma saa 24 ni kwa mujibu ya Sheria ya LATRA sura ya 413 na Sheria ya usalama Barabarani sura 168 kifungu 23 na kifungu 28 (6) madereva waliofugiwa awataruhisiwa kuendesha gari lolote Kwa kipindi chote Cha kutumikia adhabu zao.
“Ili dereva aweze kurejea atalazimika kuzingatia matakwa ya Sheria ya usalama Barabarani sura ya 168 kifungu cha 23 na kifungu 28 (6)”amesisitiza
Aidha amesema baada ya kutumia adhabu hiyo dereva atatakiwa kuomba kufuguliwa atalazimika kutathiminiwa Ili kupima uwezo wake katika taaluma yake.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani SACP Ramadhani Ng’anzi amesema madereva ambao watakuwa wakienda kinyume watafugiwa ikiwemo kufikishwa mahakamani na kufutiwa leseni.
Amesema madereva hao 10 wamefugiwa kati mwezi mmoja hadi sita kutokana na kuchezea mfumo wa VTS na mwendokasi jambo ambalo ni hatari linaweza kusababisha ajali.
“Dereva yoyote anayechezea mfumo wa VTS na tukagundua tutakufungia lakini kifungo kikiisha utafanyiwa majaribio tukiona umeshindwa majaribio utarudi ukaendeshe power Tira maana atakua hanasifa ya kuendesha gari ya abiria”amesema
Aidha kamanda King’azi amewatoa hofu wasafiri wanaosafiri usiku kwani ulinzi umeimalishwa na gari nyingi za dolia zineongezwa.
Naye katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki mabasi Tanzania TABOA, Priscus Joseph amewaomba madereva kutokwenda mwendokasi Kwa lengo la kuwahi kwani Kwa muda waliyopewa Kwa ajili ya kufanya safari hizo unatosha na hakuna haja ya kuatarisha maisha .
Pia,amewaomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na LATRA kuwashirikisha kwenye adhabu wanazotoa lakini pia Kosa la dereva lisiadhibu kampuni badala yake ahadhibiwe dereva mwenyewa.
“Nitoe rai Kwa madereva kupunguza mwendo hasa katika kipindi hiki kutokana na kuwepo Kwa mvua nyinyi nawaomba tupuguze mwendokasi hata ule wa sheria ikiwezekana upungue kwani hata barabara zitakua na maji na zinateleza”amesisitiza Joseph