Mpango mpya unajumuisha mafunzo yanayohusisha kucheza ambayo husaidia watoto kupata maarifa zaidi mbali na wayapatayo darasani.
…………………….
Cambridge, taasisi kubwa duniani inayotoa, programu za elimu ya kimataifa, imezindua mpango wake mpya wa kutoa elimu ya awali nchini Tanzania, ambao utawajengea watoto wenye umri wa miaka 3 uwezo zaidi wa kupata maarifa.
Mpango huo mpya unaohusisha njia ya michezo umeanzishwa kufuatia kuonyesha kuleta mafanikio nchini India , umetengenezwa kwa ustadi mkubwa ili kuwapatia watoto wenye umri wa miaka 3 hadi 6 mwanzo bora maishani, kuwasaidia kufikia hatua muhimu za mapema kwa kufanya vizuri katika masomo ya darasani na katika mambo mengine mbali na masomo ya shuleni.
Elimu ya awali itakayokuwa inatolewa na Cambridge itakuwa na ubora wa hali ya juu sambamba na kumwandaa mtoto mwenye umri kati ya miaka 3 hadi 19 kupata mafanikio ya kielimu.
Tafiti nyingi zinathibitisha kuwa elimu katika umri wa chini ni muhimu. Utafiti wa kimataifa uliofanywa na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) kuhusiana na Utafiti wa Kimataifa wa umuhimu wa elimu ya awali umebainisha kuwa , elimu bora na matunzo bora utotoni kwa wastani vinasaidia watoto kupata ufahamu mkubwa mara mbili ya kiwango cha kawaida.
Uamuzi wa kuboresha njia za kufundishia utaifanya Cambridge kusaidia shule nchini Tanzania na duniani kote kuimarisha utoaji wao wa elimu katika miaka ya awali, jambo ambalo inaamini litaleta manufaa kwa wazazi na walimu kadiri watoto watakavyokuwa wanafanya vizuri katika masomo yao shuleni.
Rod Smith, Mkurugenzi Mkuu wa anayesimamia elimu ya kimataifa wa Cambridge akiongea kuhusu programu hii mpya alisema, “Sote tunajua kuwa miaka ya mapema ya maisha ya mtoto ni muhimu kwa ukuaji wao. Utafiti unaonyesha kuwa kadiri tunavyosaidia watoto katika hatua hii, ndivyo tunavyoweza kuwa na matokeo chanya kwa maisha yao ya baadaye. Mpango wetu mpya wa kutoa elimu ya awali wa Cambridge, unatokana na utaalamu usio na kifani wa Cambridge katika elimu ya hali ya juu ili kusaidia shule nchini Tanzania kuwapa watoto uzoefu mwingi wa kusisimua na kujifunza kadri inavyowezekana – kutumia vyema awamu hii muhimu ya ukuaji wa ubongo na kuwafanya watoto kuanza maisha vizuri.”
Mafunzo yanayohusisha kucheza yanavyosaidia kipindi cha mpito kabla ya kuanza shule ya msingi
Mpango wa elimu ya awali wa Cambridge unatokana na utafiti wa Cambridge duniani kote juu ya kanuni za mtaala kutoka kwa mifumo ya elimu yenye ufaulu wa juu, pamoja na uchanganuzi wa utendaji bora katika elimu ya awali na sifa ambazo zina athari kubwa.
Utafiti uliwezesha kupatikana kanuni 12 muhimu ambazo zinalenga kufanikisha mpango huo. Kanuni hizo zilitengenezwa kwa ushirikiano na wasomi wa kiwango cha kimataifa, watafiti na watendaji katika elimu ya miaka ya awali. Umuhimu wa kujifunza kwa msingi wa mchezo, na hitaji la kuwasogeza watoto hatua kwa hatua kuelekea ufundishaji rasmi zaidi katika utayari wa elimu ya msingi, ni kanuni mbili zilizoongoza maendeleo ya kila kipengele cha programu. Kanuni hizo zinahakikisha kwamba watoto sio tu wanapata ujuzi kuanzia wanapokuwa na umri mdogo lakini pia wanapata ujuzi muhimu kukabiliana na ulimwengu unaobadilika haraka.
Mpango wa elimu ya awali wa Cambridge unatoa muundo unaobadilika ili kusaidia maendeleo ya kila mtoto na unaweza kubadilishwa kulingana na mahitaji ya shule mbalimbali nchini Tanzania, ukitumia mbinu za ufundishaji zilizopangwa.
Nyenzo za darasani zilizoundwa mahususi na tathmini zitasaidia walimu kuelewa maendeleo ya kila mtoto huku wakikuza ukuaji wao wa pande zote mbali na masomo ya darasani .
Juan Visser, Mkurugenzi wa Kanda, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara anayehusika na elimu ya Kimataifa wa Cambridge, aliongeza kusema: “Tunajua kwamba elimu bora ya awali inaweza kunufaisha taaluma nzima ya mtoto na kwa hivyo ninafurahi kwamba tunaongeza hatua hii mpya kwenye mpango wetu wa ufundishaji wa Cambridge. – ni kile ambacho shule zimekuwa zikiomba. Mpango wetu wa elimu ya awali wa Cambridge huleta pamoja mbinu bora kutoka kote ulimwenguni na usaidizi mkubwa wa walimu. Tunataka kusaidia shule nchini Tanzania kusaidia maendeleo ya muda mrefu ya watoto na kuwasaidia kuwa tayari kwa ulimwengu.
Mambo ya kuzingatia pamoja katika kutoa ya awali
Utafiti wa Cambridge na shule kote ulimwenguni uligundua kuwa utoaji wa elimu ya awali unazingatia mambo mbalimbali ikiwemo walengwa kuchanganyika wakitokea kwenye mazingira ya rasilimali tofauti, mitaala, tathmini na mafunzo. Hili linaweza kufanya iwe vigumu kuelewa jinsi watoto wanavyoendelea au kubainisha ni mbinu gani zina matokeo bora katika ukuaji wao.
Kwa kuhakikisha vipengele vyote tofauti vinafanya kazi vizuri pamoja, Cambridge husaidia shule kuwapa wanafunzi wao elimu ya awali na yenye ubora wa kiwango cha juu .