Na Sophia Kingimali
Tume ya Haki ya Jinai imevitaka vyombo vyote vinavyohusika na haki jinai kujikita kwenye kubaini na kuzuia uhalifu.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 8,2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande wakati wa uwasilishwaji wa ripoti kwa mabalozi wa nchi tofauti na Wakuu wa Mataifa lengo likiwa kuwapitisha kwenye ripoti yao ya Tume ili kuboresha muundo na taasisi zake ambayo iliundwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan mwaka huu.
Amesema wamewambia Mabalozi wametumia kanuni gani wamewapitisha kuhusu mapendekezo muhimu migogoro ya haki jinai lakini kwenye Taasisi kuna mambo gani makubwa ambayo wameyapendekeza.
“Tukasema hapana hiyo ni nzuri sawa lakini lazima tujikite kubaini na kuzuia uhalifu ,kwa sababu mafanikio yanakwama na hakuna uhalifu ndani ya jamii kwa sababu tuna ubaini na kuuzuia siyo unangoja utendeke alafu unapambana nao,” amesema Jaji Chande.
Amesema Suala moja kubwa limejitokeza je wajikite kwenye kupigania uhalifu au kubaini na kuzuia uhalifu hivyo moja ya mapendekezo yao kwenye hizo Taasisi kubwa za haki jinai zibadilishe usukani zijikite kwenye kubaini na kuzuia uhalifu .
Amesema tume inategemea taasisi na wizara kutekeleza huku wao wakisaidia utekelezaji huo.
Amesema wanaendelea kushirikiana na UNICEF hasa katika eneo la kuhusu haki za watoto huku tume pia ikiwa imetoa mapendezo kuhusu haki hizo.
Aidha Jaji Chande amesema wamebaini hawana sera ya Taifa ya haki jinai hilo ni jambo ambalo wametoa mapendekezo yao kwenye ripoti zao zaidi ya 360 lakini sasa hivi wapo na hizo Taasisi ili zibainishe vipaumbele katika yale mapendezo yanayowahusu wao au yanawahusu wenzao lakini pia wapo pamoja nayo.
“Sasa hivi tupo na taasisi 18 tumeshaaanza sasa hivi wiki nne tupo nao kila taasisi inaandaa mpango wao na wapo hatua za kumaliza,” ameongeza.
Amesema ripoti hiyo ni fursa yao ya pili sababu walivyoteuliwa kama tume na balozi hizo na mabalozi ni baada kukabidhi ripoti na pia wameona fursa ya kuwapitisha kuhusu mapendekezo ya tume ili wapate michango yao.
Amesema na mabalozi wametoa michango mabalozi saba akiwemo balozi wa Indonesia yeye ambapo amesema sasa hivi Indonesia na Tanzania wapo katika matayarisho ya ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenda nchini humo na wanategemea kwenye ziara hiyo ushirikiano baina ya Polisi wa Tanzania na Polisi wa Indonesia kuimairishwa.
“Baada ya sisi kukabidhi ripoti kwa Mheshimiwa Rais amefanya mambo mawili mengine ikiwemo tume kuiteua upya kuwa ni kamati ya kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya tume hivyo kutoka kuwa tume tumekuwa kamati ambayo inaisaidia serikali hususani Katibu Mkuu kiongozi ili kusaidia kusimamia kila Taasisi katika Taasisi zile kumi ma nane kuandaa mpango kazi wa utekelezaji na mikakati ya utekelezaji wa mapendekezo”amesema
Aidha ameongeza kuwa tume ilikuwa na wajumbe tisa ambapo Rais ameongeza wajumbe wengine wawili na kufanya tume kuwa na wajumbe kumi na moja na wajumbe waliongezwa ni pamoja na Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba na waziri wa wizara mbalimbali wa miaka mingi George Mkuchika kwa hivyo tume hiyo imeongezewa nguvu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mabalozi,Balozi wa Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui ameipongeza tume hiyo na ameahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha amani inaendelea kulindwa nchini.