Na Sophia Kingimali
Kampuni ya National Commercial Directory ( NCD)imetoa rai kwa wafanyabiashara kusajili biashara zao ili waweze kuwafikia wateja wengi kwa wakati lakini pia kujitangaza.
Akizungumza na waandishi wa habari novemba 8,2023 kwenye Maonyesho ya teknolojia za kifedha yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NCD, Rehema Ahmed amesema kwa kutumia kitabu ambacho kimeorodhesha wafanyabiashara wote nchini wamesaidia kukuza na kurahisisha ufanyaji wa biashara.
Amesema kitabu hiko chenye orodha ya biashara kinasambazwa kwenye wizara zote,taasisi,balozi na hoteli zote nchini ili kuhakikisha hata mgeni anapokuja hapati shida kutafuta huduma anayoitaka.
“Hiki kitabu tunakisambaza ndani na nje ya nchi ili hata mgeni anapokuja hapa anataka kwenda mwanza anaangalia tu kwenye kitabu anakua anajua afikie hoteli gani na akitaka huduma anazipata bila hata ya kutoka jasho hii inasaidia kutangaza biashara zetu kimataifa lakini tunaitangaza nchi,”amesema Rehema.
Amesema kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia wamefungua mitandao ya kijamii lengo kuongeza wigo mpana wa kuwafikia wateja lakini kuongeza hamasa kwa wafanyabiashara kujiunga na kampuni hiyo.
“tumejiunga na social media pia lakini pia tunataka kufungua na application ili tuweze kuwafikia kila mtu ukizingatia sasa hivi dunia ipo kiganjani ndio maana nawashauri wafanyabiashara wengi kuja kusajili biashara zao ili waweze kuwafikia wateja wengi”amesema Rehema
Ameongeza kuwa wanamkakati wa kuhakikisha wanazifikia biashara zote zilizosajiliwa kisheria bara na Zanzibar lakini pia kupitia mitandao ya kijamii wameweza kuwafikia watu zaidi ya 600 kwa siku na wanaendelea kuongezeka.
Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo amesema wananchi wamekuwa na uelewa mdogo wa kujiorodhesha kwenye mfumo wao hivyo wanaendelea kutoa elimu kwa watu waweze kujiorodhesha.
Sambamba na hayo amesema wamefanikiwa kusambaza kitabu hiko kwenye maeno makubwa ambapo imesaidia watu kuweza kufikiwa na huduma kirahisi bila ya kutoka jasho.
“Sasa hivi Dunia ipo mkononi haupaswi kutoka jasho kufuata huduma huduma unaifikia kwa njia rahisi hivyo niwaombe wafanyabiasha ambazo halali na zimesajiliwa kisheria wajitokeze kwa wingi kuorodhesha biashara zao waweze kufikia wateja lakini pia kujitangaza ndani na nje kwani kitabu kimefika kila sehemu nchini lakini mitandao ya kijamii ipo Duniani kote”ameongeza.