NA HERI SHAABAN (ILALA)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ameitaka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kufanya kazi vizuri kwa kutumia Mapato ya fedha za ndani .
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema hayo wakati wa kuzindua magari ya Wagonjwa (AMBULANCE ) saba yaliofanyiwa ukarabati kwa fedha za mapato ya ndani magari hayo ya wagonjwa yamesambazwa vituo vya afya kutoa huduma .
“Nawaomba watendaji wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam mfanye kazi kwa weledi na ushirikiano huku mkitumia fedha za Mapato ya ndani vizuri katika utekelezaji wa majukumu yenu.” alisema Mpogolo
Mkuu wa wilaya Mpogolo alisema Ilala sasa hivi ni faraja Idara ya Afya ya Halmashauri ya Jiji imefanya vizuri pongezi kubwa zimwendee Mganga Mkuu wa wilaya Zaituni Hamza, na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jomaary Mrisho Satura ambapo watu hawakupenda yafanyike lakini kwa mapenzi mema na Serikali katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan yamefanyika ni Viongozi ambao mnaweka alama Ilala kwa kasi ya uchapakazi.
Aliwataka watumishi wa afya wa Ilala wote kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuisaidia Serikali ili malengo waliojiwekea yaweze kutimia
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Zaituni Hamza, alisema mara baada kufika Ilala alipewa maelekezo ya kazi huku akitakiwa kujipanga katika kutekeleza majukumu ya kazi na kutoa huduma bora kwa jamii ndani ya wilaya Ilala.
Mganga Mkuu Zaituni Hamza ,alisema Idara ya Afya wamekusanya pesa za kutosha ni juhudi zake katika usimamizi mkubwa kwa ushirikiano na watendaji wake na watumishi .
Alisema mikakati ya Idara ya afya Halmashauri ya jiji hilo inatarajia kufungua chuo cha Afya ndani ya wilaya Ilala.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jomary Mrisho Satura alisema magari yote saba ya wagonjwa yametengezwa kwa wakati mmoja ambapo yamegharimu shilingi milioni 24 sasa hivi yanasambazwa vituo vya afya kwa ajili ya kutoa huduma za wananchi katika sekta ya afya
Mkurugenzi Jomary Mrisho Satura aliwataka watumishi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam katika sekta nyingine kujifunza Sekta ya afya mikakati yao ili na wao waweze kufikia malengo Ilala iweze kusonga mbele katika idara zote.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde, alimpongeza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kwa utendaji bora wa kazi na ubunifu ambapo aliwataka wakuu wa Idara wa Halmashauri ya jiji kuiga mfano mfano huo na ubunifu aliotumia,huku akiwataka madereva waliopewa dhamana kusimamia magari hayo kuyatunza .