Na Sophia Kingimali
Serikali imekitaka clChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kinahakikisha ujenzi wa kampasi mpya ya chuo hicho mkoani Kigoma unakuwa na tija na maslahi kwa taifa.
Hayo yameelezwa leo Novemba 6, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Dkt Kenneth Hosea akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wenye lengo la kujadili mapitio ya mitaala ya chuo hicho lakini pia uanzishwaji wa kampasi mpya mkoni Kigoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa HEET.
Amesema serikali imeendelea kuiwezesha sekta ya elimu inayoinua na kukuza ubora wa elimu nchini.
Kupitia mradi wa HEET (Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi) serikali imeboresha mitaala ,rasilimali watu na mazingira ya kufundishia katika vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimu ya juu 23.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nimpongeze sana kwani ameendelea kuiwezesha elimu nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali inayolenga kuchechemua sekta ya elimu huu mradi wa HEET unatekelezwa chini ya ufadhili wa mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Dunia”amesema Dkt Hosea.
Amesema mradi huo utaboresha miundombinu ya TEHAMA na kujenga ndaki ya tiba katika kampasi ya Mloganzira na kuanzisha kampasi mpya ya Kigoma.
Amesema uanzishwaji wa kamapasi ya Kigoma unapaswa uvutie wagonjwa kwenda kupata tiba lakini pia kupata matibabu hiyo itasaidia nchi kuendelea kujitangaza katika huduma na kutanua soko.
Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema mkutano huo unatarajiwa kuja na maoni ambayo yatasaidia kuboresha mitaalam hiyo ili wahusika wanapofundishwa kupitia mitaala hiyo waweze kuendana na uhitaji wa soko.
Amesema kabla mitaala haijapata ithibati inapaswa kupitiwa na kutolewa maoni ili kusudi inapokwenda kutumika kwenye kufundishia iweze kukidhi haja ili wataalum wakihitimu waweze kutoa huduma inayohitajika,
“Tunashirikisha wadau kutoa maoni kuhusu mitaala ya chuo ya masomo ya uzamili ambapo mpaka sasa tumepitia mitaala 79 sasa zoezi lote tumeshalifanya leo tumeleta tujadili kwa pamoja mitaala yote tuliyopitia na maoni yaliyotolewa ni yale ambayo wote tunayahitaji”amesema Kamuhabwa.
Akizungumzia uanzishwaji wa kampasi ya Kigoma amesema tayari wameshaandaa andiko na ramani ya chuo kitakavyokuwa hivyo wamewashirikisha wadau ili kuona namna ambavyo wataboresha ili chuo hico kiwe na manufaa makubwa kwa ukizingatia kuwa mkoa wa Kigomo hauna chuo kikuu.
Naye,Mratibu wa mradi HEET MUHAS Dkt Nathanael Sirili amesema uanzishwaji wa kampasi ya Kigoma umeangalia zaidi soko la nje kwa nchi ambazo zipo magharibi mwa upande wa kiggoma kama Congo,Burundi,Rwanda na nchi nyingine.
Amesema Muhimbili wamekuwa na wanafuzi wa kutoka nchi nyingine mbalimbali lakini si Kongo wala Burundi hivyo wanatarajia uanzishwaji wa kamapsi hiyo utakua na tija kubwa.
“kama tunavyofahamu nchi ya Congo huwa inakubwa mara kwa mara na magonjwa ya mlipuko kama Ebola kwa hiyo tunajaribu kukusanya maoni ii kutengeneza programu zitakazojibu changamoto hizo”amesema.
Amesema tayari wana bilioni 36 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kampasi hiyo ambapo pesa hizo ni kwaajili ya kuanza kujenga baadhi ya miundombinu.
“Tunategemea Kigoma na yenyewe utaanza taratibu kama ilivyoanzishwa chuo kikuu hapa kwa sababu ni juhudi za serikali kitakamika kwa wakati na elimu kuanza kutolewa”ameongeza.
Kampasi ya Kigoma inatarajiwa kuanza kazi rasmi 2026/2027 ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza 2024 na utachukua miezi 24.