Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka kubwa la Hisense lililofunguliwa Mtaa wa Azikiwe jijini Dar es Salaam leo.
Meya wa Jiji la Ilala Omary Kumbilamoto akitoa salam zake katika uzinduzi huo wa duka la Hisense uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara Bi. Sabaha Said akizungumzia namna duka hilo la Hisense linavyouza vifaa vyenye ubora wa juu na kuwataka wananchi kwenda kununua vifaa vya majumbani vya Hisense katika duka hilo.
…………………………………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Serikali ya Awamu ya Sita imesema itaendelea kudumisha amani na usalama wa Taifa pomoja kutengeneza mazingira rafiki ya biashara jambo ambalo litasaidia kuongeza kasi ya wadau wa maendeleo kuja nchini Tanzania kufanya uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Akizungumza leo Novemba 6, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa duka la vifaa vya umeme la Hisense Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani ameifungua nchi na kuifanya kuwa sehemu salama ya kufanya uwekezaji.
Mhe. Mpogolo amesema kuwa duka la Hisense litakuwa linauza vifaa vinavyoendana na Teknolojia ya kisasa jambo ambalo litasaidia kuwa na bidhaa Bora Tanzania.
“Hisense wamekuwa wakiuza bidhaa zenye ubora na gharama nafuu, wakati umefika kwa Tanzania kuchangia fursa ya kupata bidhaa zenye ubora” amesema Mhe. Mpogolo.
Amesema kuwa Hisense wanatambua Tanzania ni sehemu salama ya kufanya biashara kutokana mazingira mazuri tafauti na nchi nyengine.
Mhe. Mpogolo amesema kuwa watanzania wanapaswa kuja katika duka la Hisense kwa ajili ya kujifunza namna ya kutengeneza mazingira mazuri ambayo yanaweza kushawishi wateja.
“Hisense ni wafanyabiashara wazuri ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu lao la kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa” amesema Mhe. Mpogolo.
Nae Mfanyabiashara Bi. Sabaha Said, amesema kuwa kuwa bidhaa za Hisense inaongoza kwa ubora na teknolojia rafiki kwa matumizi mbalimbali.