Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Taifa Paul Makonda .
……..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katibu wa NEC Siasa,itikadi na uenezi Taifa na mjumbe wa kamati kuu Paul Makonda, atapewa uchifu katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kutokana na utendaji kazi wake mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ikiwemo kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 6, 2023 na Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Mwanza Prudence Sepa wakati akitoa ratiba ya ziara ya kikazi ya Katibu huyo itakayoanza Novemba 11-13 mwaka huu.
Sepa amesema wananchi wa misungwi wamefurahishwa na utendaji kazi wa Katibu huyo ndio maana wameamua kumpa heshima hiyo ya uchifu ili
Imsaidie katika shughuli zake kama kiongozi wa kitaifa.
Aidha, ameeleza kuwa katika ziara hiyo Katibu wa NEC siasa, itikadi na uenezi atakagua maendeleo ya mradi wa daraja la Kigongo Busisi atazungumza na wazee wa Mkoa wa Mwanza na kamati ya amani pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambapo atasikiliza kero za wananchi.