Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuhakikisha mipango ya Sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya inafanikiwa kwa uweledi mkubwa kwa kusimamia huduma ziweze kuwafikia wananchi katika maeneo tofauti.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo katika Hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwenye Mkutano Mkuu wa Nne (4) wa Chama Cha Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba Saidizi (APOT) unakwenda sambaba na kilele cha siku ya Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba saidizi Duniani uliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul- Wakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya ina dhmana kubwa ya kusimamia masuala yanayohusu watu wenye ulemavu wa viungo, uhitaji wao na kuhakikisha huduma bora zinawafikia kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo wana