Na Sophia Kingimali
Umoja wa Jumuiya ya Wanawake CCM UWT wilaya ya Kinaha mkoani Pwani wamepongeza juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwainua wananchi hasa wanawake katika mkoa huo.
Hayo yameelezwa na mllMwenyekiti wa UWT Kibaha Elina Mgonja wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mkoa hapo.
Amesema mkoa wa Pwani sasa umepata huduma zote muhimu kwani kila kata imekua na shule ambapo watoto wanasoma lakini pia hospitali jambo ambalo limeondoa changamoto kwa wanawake kujifungulia nyumbani na njiani kutokana na umbali wa hospitali au vituo vya afya.
“Kiukweli sisi wanawake kibaha tunampongeza na kumshukuru sana Rais Dkt. Samia sasa hivi tuna hospital,tuna shule kwenye kila kata watoto wetu wanasoma lakini pia barabara kila sehemu hii imepelekea hata uchumi wetu kukua”amesema Mgonja.
Amesema Rais amefanya kwa vitendo mambo yote ambayo ndio uhitaji mkubwa wa wananchi na kusaidia wanawake kupunguza utegemezi kwani amesaidia kuwainua wanawake kiuchumi.
Aidha Mgonja amempongeza mbuge wa jimbo hilo Francis Koka kwa kuwa karibu na wanawake na kuwawezesha kwa kuwajengea jengo la biashara litakalowasaidia kufanya shughuli zao za kijasiliamali.
“Kwa namna ya pekee sana naomba nimpongeze na kumshukuru mbunge wetu kwani amefanya jambo la kukumbukwa sana kwenye mioyo ya wanawake maana jengo hili tutalitumia kama kituo cha bidhaa za wajasiliamali”amesema Mgonja.
Amesema jengo hilo la biashara lililojengwa na mbunge linatarajiwa kuzinduliwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa mama Merry Chatanda.
Aidha Mgonja ameongeza kuwa wanawake wa mkoa huo wameweka mkakati ambao utakua endelevu wa kupita nyumba kwa nyumba mtaa kwa mtaa na ofisi kwa ofisi ili kuelezea mazuri yanayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt. Samia katika kuliletea taifa maendeleo.