Na Sophia Kingimali
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla ametoa wito kwa wadau wa TEHAMA wakiwemo wakuu wa shule za awali msingi na sekondari wahamasike kuanzisha klabu za kidijiti lakini wahakikishe wanafuata misingi na maadili ya nchi.
Akizungumza Novemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kitabu Cha uanzishwaji na uratibu wa Klabu za kidijiti amesema kuanzishwa kwa kitabu hicho ni muongozo wa vijana kupata fursa ya mapinduzi ya kidijiti.
Katibu Mkuu amesema ,kupitia kitabu hicho kitaleta dira chanya ya ubunifu kwenye nchi.
“Sera ya mwaka 2016 ipo kwenye mchakato wa Kubadilishwa ambapo katika mchakato huo tumeweka kipengele cha kuchochea talanta na kuandaa sera ya kampuni changa ambayo itawasaidia baadaye kuwa na wadau wakubwa,”amesema
Amesema kujenga Taifa la kidijitali kupitia Klabu hizo zitachangia ufumbuzi na kuwawezesha vijana kuwa wabunifu na wajasiliamali kupitia TEHAMA.
Pia amesema uwanzishaji wa vituo vya ubunifu nchi nzima bila kujali elimu waliyonayo kutasaidia kuongeza ajira nchini.
“Kwa Kujifunza TEHAMA itawasaidia kuwa Bora zàidi na kukuza uchumi na kusaidia mikakati ya kukuza uchumi,”amesema
Hata hivyo amesema Wizara itaongoza safari hiyo ya kidijitali ili nchi ifike katika uchumi ya kidijiti.
Awali Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt.Jabir Bakari amesema klabu za kidijiti ni majukwaa ya hiari yanayowakutanisha wanafunzi wa rika moja kupata uelewa na kuhamasishana juu ya tehama uchumi kidijiti na fursa zake.
“Kupitia klabu hizi za kidijiti tunajenga jamii yenye ufahamu wa teknolojia ya kidijiti na iliyo na taarifa na fursa zake “amesema Dkt Bakari
Dkt. Bakari amesema lengo la uwekezaji kwenye tehama ni kuboresha na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma Kwa wananchi na kuongeza uwezo wa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchumi kidijiti.
Ameongeza kuwa dunia ipo katika zama za taarifa zinazoenda sambamba na uchumi wa kidijiti .
“Katika zama hizi ambazo zinajulikana kama zama za mapinduzi ya nne ya viwanda tehama ndiyo nyazo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.