Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier amewasili nchini leo tarehe 30 Oktoba 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba 2023, na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikabidhiwa maua alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |