Na Sophia Kingimali.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege nchini ili visiwe vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu ili nchi iendelee kuwa na sifa ya kati ya nchi zenye udhibiti wa anga.
Pia ameitaka Bodi ya Mikopo kufanya marejeo ya viwango vya mikopo vinavyotolewa kwa wanafunzi wa urubani ili kutoa kipaumbele kwa wahitaji wa fani za masuala ya usafiri wa anga.
Maagizo hayo ameyatoa jijini Dar es Salaam Oktoba 30 katika maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003 pamoja na kuzindua Women Aviation kwa malengo mbalimbali ikiwa kidhibiti na kusimamia huduma za usafiri wa Anga nchini.
“TCAA imarisheni mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege ili kuhakikisha haviwi vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu nchi iendelee kuwa na sifa ya kuwa kati ya nchi zenye udhibiti wa anga ,” amesema Majaliwa .
Majaliwa ameitaka Mamlaka hiyo kujifunza kutoka Kwa mataifa yaliyofanikiwa ili kuongeza viwango vya utoaji wa huduma na kuwa wabunifu wa hali ya juu kwa kuwa na mikakati ya kuimarisha soko ili nchi isiachwe nyuma kimaendeleo.
Pia amewataka wadau wa usafiri wa anga nchini, kutekeleza majukumu yao Kwa kufuata Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamiwa masuala ya usafiri wa anga kitaifa kwa ajili ya kuhakikisha usalama na kipaumbele namba Moja katika usafiri wa anga.
Vilevile ameitaka TCAA kubuni na kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya ‘Aviation Training Fund ‘ ili kuongeza idadi ya marubani wanaopata ufadhili wa masomo.
“Watanzania endeleeni kuviamini na kutumia vyuo vilivyopo nchini kwani vinatoa mafunzo ya utalaamu wa anga wa uhakika.
Majaliwa amesema serikali imepanga kuimarisha sekta ya anga kwa kuwezesha ununuzi wa rada za kisasa nne za kuongoza ndege za kiraia ambazo zimefungwa katika viwanja vya ngege vya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.
“Hivi karibuni, viwanja vya ndege vya KIA, Zanzibar na JNAI vilikaguliwa na kupata asilimia 86.7 hatua hiyo imeowezesha nchi yetu kushika nafasi ya nne badani Afrika ikitanguliwa na nchi ya Nigeria ,Kenya, Ivory Cost, huu ni ushindani tosha kwamba uwezo wa nchi yetu katika kidhibiti usalama wa anga unaendelea kuimarika,”amesema.
Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewapongeza TCAA Kwa kusimamia ukaguzi huo na kuiweza nchi kupata alama 86.7 katika kiwanja cha Dar es Salaam na Zanzibar.
Amesema serikali imeboresha miundombinu mbalimbali ya viwanja vya ndege hivyo kutokana na maboresho hayo anaamino ukaguzi ujao nchi itafikia asilimia 90.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCCA, Hamza Johari, amesema kuwa Mamlaka hiyo inaendeshwa Kwa kutumia mapato ya ndani na haitegemei ruzuku kutoka serikali.
“Kwa miaka mitano tumekusanya bilioni 319.9 na bilioni 24.5 tumepeleka serikalini kwa ajili ya kumechangia katika mambo mbalimbali ya kijamii,”amesema Johari
Amesema TCCA inaendelea kufungua mikataba mbalimbali ya usafiri Kwa nchi 80 hivi karibuni wameingia mkataba na nchi ya Marekani hivyo kuziwezesha ndege ya Air Tanzania kufanya safari kwenda kwenye nchi hiyo.
“TCCA wataacha kusomesha marubani nje ya nchi na kusomesha kwenye Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT) Kwa mwaka tulikuwa tunapeleka marubani 10 nje ya nchi sasa tunasomesha marubani 30 nchini na fedha kubaki nchini,”amesema.