Na Ahmed Mahmoud
Waziri wa Maliasili na Utalii Anjela Kairuki amesema kuwa Mkutano unaondelea Jijini utakuwa na manufaa makubwa kwa Wataalamu wa Bara la Afrika na Tanzania watanufaika na fursa ya majadiliano mahususi ya biashara hewa ukaa.
Aidha soko la hewa Safi ya Kaboni lililopo ni fursa muhimu kwani Dunia inaelekea huko katika kuboresha Anga kutokana na madhara ya uharibifu wa hewa chafu ya kabon katika kuhakikisha tunaokoa anga kuondokana na ongezeko la Joto duniani.
Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 24 wa kamisheni ya Afrika inayosimamia Misitu pamoja na wanyamapori kutoka nchi 53 ukiongozwa na Shirika la chakula na Kilimo la Umoja FAO unaondelea Jijini Arusha kwa siku Tano.
Amesema Mkutano huo umeanza kufanyika tokea miaka ya 1960 na hii ni takribani miaka 63 ndio Tanzania inapata fursa ya kufanyika Mkutano huo wa kamisheni hapa nchini ni heshima Kubwa kwetu na Mkutano huu zaidi ya nchi 40 zimeshatuma wawakilishi wao ukiwa na washiriki 300.
“Kama mnavyojua TFS imeendelea kufanya majadiliano na wadau katika biashara ya hewa ukaa lakini pia tunaangalia hifadhi zetu Wana Misitu wanaweza kupanda miti ikatunzwa ikahifadhiwa bila kukatwa na bado ukalipwa fedha kutoka kwa wawekezaji Duniani wenye mapenzi mema na biashara ya hewa ukaa”
Kwa Upande wa Kamishna wa Wakala wa Misitu nchini TFS Prof. Dosantos Silayo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa Kamisheni hiyo amesema kwamba Mkutano huo 24 na nchi 40 zinashiriki wakiongozwa na nchi zingine na mawaziri wakurugenzi wa sekta za Misitu ambapo washiriki wengine wanashiriki kwa njia ya Mtandao.
Amesema majukwa kama haya ni kutoa fursa za kubadilisha uzoefu katika Usimamizi wa rasilimali za Misitu na wanyamapori lakini pia kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za sekta hizo kwani zinakabuliwa na changamoto kadhaa ikiwemo Mabadiliko ya tabianchi kwani mataifa ya Afrika yanapaswa kuweka mikakati ya pamoja kwa sababu rasilimali hizi zinavuka mipaka.
Awali Mkurugenzi wa Idara za Misitu SMZ Said Juma Ally wakati serikali ya awamu ya nane ikijikita kwenye uchumi wa bluu kwenye Yale Mazao 5 wanashirikiana na Jamii katika utunzaji wa kuzalisha bluu Kaboni kutokana na Mazao ya Mikoko ambayo Kuna maeneo yametunzwa na serikali na watu binafsi.
Amesema ukichukuwa data za mwaka 1997 ukilinganisha na Sasa ikiwemo tathmini ya mwaka 2013 utakuta hekta zaidi ya 3000 zimepungua kutokana na matumizi mbalimbali kwani kupungua kwake Kuna athari Kubwa kwa uchumi wa bluu ikizingatiwa Mikoko ndio inafyonza kila kitu.
Hata hivyo akiongea kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti wizara ya Kilimo Maliasili na Umwagiliaji Zanzibar Makame Kitwana Makame amesema wamekuja kutoa mchango wao kama SMZ hasahasa kuunganisha Jukwaa hili na uchumi wa bluu hususani katika uhifadhi wa rasilimali za mikoko ambayo ni hekta 17 kwa Zanzibar.
Amesema Moja ya rasilimali zenye changamoto Kubwa katika uhifadhi ni Mikoko hasa kwa zile ambazo zipo kwenye maeneo ambayo hayajatambuliwa kuwepo kwenye hifadhi ya serikali ambapo tuna hifadhi za aina mbili za serikali na hifadhi za wanajamii ikiingia huko inakuwa imepata hifadhi Kubwa.